Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-CHIBOK

Boko Haram yarusha video mpya inayoonyesha "Wasichana wa Chibok"

Boko Haram imerusha hewani video mpya Jumapili ya wasichana kama wale wa shule ya sekondari ya mjini Chibok waliyotolewa na kundi la wanajihadi nchini Nigeria mwezi Aprili 2014 mjini Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Video hii iliyorushwa Agosti 14, 2016kwenye Youtube inaonyesha mwanachama wa tawi la kijeshi la Boko Haram akiwa pamona wasicahana ambapo wazazi wa wanafunzi wasichana waliotekwa nyara katika shule ya Chibok wamewatambua kama binti zao.
Video hii iliyorushwa Agosti 14, 2016kwenye Youtube inaonyesha mwanachama wa tawi la kijeshi la Boko Haram akiwa pamona wasicahana ambapo wazazi wa wanafunzi wasichana waliotekwa nyara katika shule ya Chibok wamewatambua kama binti zao. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Boko Haram limesema wasichana hao wanaweza kuachiliwa iwapo wapiganaji wake wanaozuiliwa jela wataachiliwa huru.

Mmoja wa wasemaji wa vuguvugu linalotetea kuachiliwa kwa wasichana hao "Bring Back Our Girls" (BBOG), Abubakar Abdullahi, tayari ameliambia shirika la habari la AFP kwamba angalau mmoja wa wasichana walioonyeshwa kwenye video, ametambuliwa kama mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chibok. "Bado tunajaribu kuwatammbua wasichana wengine wengi walioonyeshwa kwenye video hiyo," Abubakar Abdullahi ameongeza.

Aprili 14, 2014, kundi la Boko Haram liliwateka nyara wasichana 276 katika shule ya sekondari ya wasichana ya mjini Chibok. Hali hiyo ilizua hasira nchini Nigeria na duniani kote.

Wasichana hamsini na saba kati yao walifanikiwa kutoroka katika masaa yaliyofuatia baada ya kutekwa nyara na kundi hilo, ambalo jina lake ni "Boko Haram" maana yake "elimu ya Magharibi ni dhambi" katika lugha ya Kihausa, na ambalo lengo lake ni kuundwa kwa Dola la Kiislamu. Video ya kwanza ya inayoonyesha wasichana wa mji wa Chibok ilirushwa hewabi na Boko Haram mwezi Mei 2014.

"Wanapaswa kutambua kuwa watoto wao bado mikononi mikononi mwetu"

Katika video hii mpya ya dakika 11 iliyorushwa kwenye mtandao wa YouTube, anaonekana mtu anayejificha uso, akisema : "wanapaswa kujua kwamba watoto wao wako mikononi mwetu."

Akivalia sare ya kijeshi, silaha kifuani, mtu huyo anasimama katikati ya kundi la wasichana kadhaa. Wasichana wote wamevaa hijabu na abayas (gauni ndefu nyepesi na laini). Baadhi wanakaa, wengine wamesimama nyuma ya wengine.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.