Pata taarifa kuu
LIBYA-IS

Wapiganaji wa IS watimuliwa Sirte

Majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA) yenye makao yake mjini Tripoli, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, yametangaza kuwa yamedhibiti makao makuu ya kundi la Islamic State katika mji wa Sirte.

Wapiganaji wa vikosi ninavyounga mkono serikali katika mji wa Sirte, Julai 31, 2016.
Wapiganaji wa vikosi ninavyounga mkono serikali katika mji wa Sirte, Julai 31, 2016. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Vikosi hivyo vikiongozwa na wapiganaji wa mji jirani wa Misrata, vimesema vinadhibiti kituo cha mikutano cha Ougadougou na hospitali kuu ya Sirte, lakini bado baadhi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State wapo katika makazi ya watu katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Reda Issa, msemaji wa operesheni hiyo, wapiganaji 40 wa kundi la IS wameuawa, wapiganaji wengine wa kundi hilo wamekimbilia maeneo mengine ya Sirte, ambayo wanadhibiti.

Msemaji huyo ameeleza kuwa ndege za Marekabi ziliendesha Jumatano hii mashambulizi ya anga matatu. Mashambulizi hayo yalilengwa magari matatu yaliyokua yametegwa mabomu na kundi hilo la kijihadi. Lakini amekataa kusema kama vikosi vya Marekani au Uingereza vimeingilia kati mashambulizi ya nchi kavukwa upande wa wapiganaji wa Libya mjini Sirte. Amebaini kwamba wapiganaji 2500 wanapambana dhidi ya kundi la IS katika mji wa Sirte.

Jumatano usiku, kundi la Islamic State lilikua bado likidhibiti maeneo manne ya muhimu mjini Sirte.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.