Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: watu zaidi ya 70 wauawa, polisi yanyooshewa kidole

Vikosi vya usalama vya Wthiopia vinatuhumiwa kutumia nguvu zaidi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70 katika maandamano yaliyofanyika mwishoni mwa juma lililopita katika majimbo ya Oromo na Amhara, makabila makuu mawili nchini humo.

Askari polisi akijaribu kuwatuliza waandamanaji waliokua wakiandamana dhidi ya serikali ya Ethiopia, Agosti 6, 2016.
Askari polisi akijaribu kuwatuliza waandamanaji waliokua wakiandamana dhidi ya serikali ya Ethiopia, Agosti 6, 2016. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limetoa ripotia Jumatatu hii Agosti 8 ambapo limebaini kwamba watu 100 waliuawa katika maandamano hayo na zaidi ya 110 walijeruhiwa.

Kiwango cha matukio ya mwishoni mwa wiki ya Agosti 6 na 7 na na idadi ya vifo vimeanza kuibua hali ya sintoifahamu nchini Ethiopia.

Mikusanyiko na maandamano viilifanyika Jumamosi Agosti 6 katika jimbo linalokaliwa na watu kutoka kabila la Oromo, ambalo ni kabila linaloongoza kwa watu wengi nchini humo. Wakati huo ploisi ilitumia nguvu za kupita kiasi kwa kuvunja maandamano hayo. Katika vijiji kadhaa, polisi iliwapiga waandamanaji risasi za moto.

Maandamano hayo,kwa mara ya kwanza, yalishuhudiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa, ambapo waandamanaji mia kadhaa walitawanywa kikatli.

Wahanga kadhaa katika jimbo la Amhara

Siku ya pili, Jumapili, Agosti 7, maandamano yalisambaa hadi katika jimbo la Amhara, kaskazini mwa nchi, pamoja na maelfu ya watu katika mji wa kitalii wa Bahir Dar. Katika mji huo, kulishuhudiwa makabiliano kati ya waandamanaji na polisi, ambayo yalisababisah vifo vya watu kadhaa.

Serikali ya Ethiopia pia ilitaka kuzuia madhara ya wimbi hili la maandamano na kukata kabisa mawasiliano ya simu na mitandao kwa karibu masaa 48 nchini kote.

Oromo na Amhara, makabila mawili makubwa nchini Ethiopia yanaandamana kwa miezi kadhaa kwa sababu mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.