Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA

Sinai: jeshi la Misri latangaza kumuawa kiongozi wa "IS Misri"

Douaa Abu al-Ansari, kiongozi wa tawi la kundi la Islamic State katika eneo la Sinai, ameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Misri, mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vya watu 45. Zamani likishirikiana na kundi la al-Qaeda, kundi la Ansar beit al-Maqdess liliamua kushirikiana na kundi la Islamic State mwaka 2014.

Kituo cha ukaguzi wa jeshi katika mji wa el-Arish kaskazini mwa eneo la Sinai, Julai 15, 2013, ambapo basi lililokuwa likisafirisha wafanyakazi liliposhambuliwa kwa roketi, na kuua angalau watu 3  na kuwajeruhi wengine 17.
Kituo cha ukaguzi wa jeshi katika mji wa el-Arish kaskazini mwa eneo la Sinai, Julai 15, 2013, ambapo basi lililokuwa likisafirisha wafanyakazi liliposhambuliwa kwa roketi, na kuua angalau watu 3 na kuwajeruhi wengine 17. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kwenyeukurasa wake wa Facebook, jeshi la Misri lilitangaza Alhamisi, Agosti 4 kwaba limmua Douaa Abu al-Ansari, kiongozi wa wa tawi la kundi la Islamic State (IS) katika eneo la Sinai. Kundi hili la kijihadi linalojulikana kwa jina la Ansar Beit al-Maqdess kwa lugha ya Kiarabu, limekua likiendesha mashambulizi yanayolenga hasa vikosi vya usalama kwa zaidi ya miaka mitatu. Douaa Abu Al-Ansari pamoja na wengi miongoni mwa maafisa wake wasaidizi muhimu waliuawa katika mashambulizi yaliyoendeshwa na jeshi kaskazinii mwa eneo Sinai.

Kundi la Ansar Beit al-Maqdess ambalo lnahusuka na mashambulizi mengi katika eneo la Sinai, awali lilijiunga na kundi la al Qaeda, na mwaka 2014 liliamua kujiunga na kundi la Islamic State. undi hili lilijinasibu "Mkoa wa Sinai" ili kuonyesha kuwa limejiunga na "uongozi" uliotangazwa na wanajihadi wa kundi la Islamic State katika maeneo wanayoyadhibiti nchini Syria na Iraq.

Kifo ambacho ni vigumu kuthibitisha

Jeshi la Misri pia limesema katika taarifa yake kwamba zaidi ya wanachama 45 wa kundi la slamic State waliuawa na wngine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyoendeshwa dhidi ya maficho ya kundi hili kusini na kusini magharibi mwa mji wa Al-Arish, mji mkuu wa jimbo la Sinai Kaskazini. Ndege za kivita aina ya F16 na helikopta za kijeshi zilitumia katika operesheni hii. Jeshi la Misri limetangaza mara kadhaa kwamba limewaua viongozi wa kundi hilo, lakini ni vigumu kuthibitisha taarifa hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.