Pata taarifa kuu
MISRI

Sisi apongeza mapinduzi yaliyomuondoa Morsi madarakani

Rais wa Misri, jenerali Abdel Fatta al-Sisi, amepongeza na kuyaita ni “Mapinduzi”, maandamano yaliyofanyika nchini humo na kupelekea kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa Kiislamu, mtangulizi wake Mohamed Morsi.

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi REUTERS/Hassan Ammar/Pool
Matangazo ya kibiashara

Al-Sisi amesema haya wakati wa maadhimisho ya tatu ya maandamano hayo, ambapo mamilioni ya raia waliandamana kwenye viunga vya jiji la Cairo na miji mingine, June 30, mwaka 2013, kushinikiza kuondoka madarakani kwa Mohamed Mosri, ambaye utawala wake wa mwaka mmoja ulikosolewa vikali.

Sisi ambaye wakati huo alikuwa mkuu w amajeshi, alimpa Morsi saa 48 kuwa ametekeleza matakwa ya wananchi, kabla ya kuagiza jeshi kumpindua na kumuweka kizuizini.

Rais al-Sisi amewaambia wananchi kuwa, nchi yao inasherekea mapinduzi, mapinduzi ambayo wananchi wa Misri wamepata utambulisho wao na kurekebisha njia wanayoelekea na kuithibitishia dunia kuwa kamwe hawawezi kuminywa wala kutawaliwa kiimla.

Toka kuondolewa madarakani kwa Morsi, zaidi ya waandamanaji elfu 1 wamekufa, wakiwemo watu zaidi ya 600 waliokufa kwenye siku moja ya Agasti 14 wakati polisi walipowasambaratisha waandamanaji jijini Cairo wakishinikiza Morsi kurejeshwa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.