Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Ufaransa: Mmoja wa waandamanaji wanaovalia vizibao vya njao afariki baada ya kugongwa na lori Avignon
 • Raia wa pili wa Canada akamatwa nchini China
 • Uturuki: Watu wanne wapoteza maisha na 43 wajeruhiwa katika ajali ya treni Ankara (gavana)
 • Jerusalemu: Mshambuliaji avamia polisi wawili wa Israel kabla ya kuuawa (polisi)
 • DRC: Ghala la Tume ya Uchaguzi lateketea kwa moto siku kumi kabla ya uchaguzi (mamlaka)
Afrika

Wanamgambo 10 wauawa katika mapigano na jeshi Ituri

media Mambasa, Province de l’Ituri, RD Congo. Des policiers congolais en formation à la sécurisAskari polisi wa DRC wakiwa katika mafunzo ya kutoa ulinzi na usalama wa uchaguzi kwa msaada wa MONUSCO. Mambasa, jimbo la Ituri, DRC. Photo MONUSCO/Anne Herrmann

Wanamgambo 10, wakiwemo wanawake wawili, wa kundi la waasi la FRPI wameuawa na askari wawili kujeruhiwa vibaya katika mapigano yaliyotokea Jumatatu hii Juni 27 katika kijiji cha Kienge wilayani Walendu Bindi kati ya kundi hilo na jeshi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi, ambavyo vimetoaripoti hii, mapigano yalianza wakati majeshi ya DRC (FARDC) yalipoanza operesheni ya kuvunja ngome za wanamgambo wanaotafuta kujipanga vizuri kwa zaidi ya wiki moja katika mkoa huu wa jimbo la Ituri.

Naibu mkuu wa eneo la kijeshi la FARDC katika jimbo la Ituri amesema kwamba waasi hao wanajaribu kujipanga vizuri ili kuendelea kuhujumu raia.

Baada ya zaidi ya saa tatu ya mapigano, afisa huyo amesema, bunduki tatu aina ya AK 47 zilikamatwa na jeshi na kuwadhibiti wapiganaji wawili.

Chanzo kimoja kinasema kwamba wawili kati ya wapiganaji hao wamejeruhiwa vibaya.

Aidha, vyanzo vya ndani vinaarifu kwamba kundi jingine la wanamgambo liliingia katika kijiji cha Sidabo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu hii.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka arobaini amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi. Mali kadhaa pia ziliibiwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana