Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI

Moise Katumbi aombewa kufungwa miaka 5 jela

Afisa wa mashitaka ameombea hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela dhidi ya Moise Katumbi, Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga. Anatuhumiwa kupokonya na kuuza nyumba ya Bw Alexandros Stoupis, raia wa Ugiriki.

Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi,wakati akihojiwa Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi,wakati akihojiwa Lubumbashi, Juni 2, 2015. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii ilisikilizwa, Jumatatu, Juni 20, katika mahakama ya mjini Lubumbashi (Haut-Katanga).

Wanasheria wa Moise Katumbi, waliokuwepo wakati wa kesi hiyo, hawakuruhusiwa kuwakilisha mteja wao, ambaye yupo kwa wiki tatu Ulaya kwa ajili ya matibabu.

Mahakama imetoa hoja kwamba wakati mtuhumiwa anakabiliwa na kosa, ambalo adhabu yake ni zaidi ya miaka mitano, kuripoti kwake mahakamani kunahitajika.

Kutokana na kutokuwepo kwa Moise Katumbi, mahakama ilianza na kufunga uchunguzi wa kesi.

Upande wa mashtaka waliomba adhabu ya kifungo cha miaka 5 dhidi ya Moise Katumbi, wakati ambapo hukumu rasmi inatarajiwa ndani ya muda wa siku nane.

Mashitaka hayo yamekua mwezi mmoja baada ya mgombea kutangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwaka huu. Awali alishitakiwa kwa kosa la "kuhatarisha usalama wa taifa" na kuwekwa chini ya kibali cha kukamatwa kwa muda. Kibali hiki kilitokewa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri.

Katika kesi hiyo, alishtakiwa kuajiri mamluki wa kigeni kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa.

Pamoja na hukumu hiyo, Moise Katumbi alipa ruhusa kutoka kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri kufanyiwa matibabu nje ya nchi.

Mkuuwa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga alisafirishwa tarehe 20 Mei nchini Afrika Kusini kwa matibabu. Moise Katumbi aliondoka Afrika Kusini Mei 28 akielekea Ulaya kuendelea kupata matibabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.