Pata taarifa kuu
DRC

Hukumu ya Bemba kujulikana Jumanne

Majaji katika makahama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC siku ya Jumanne wanataraji kutoa hukumu kwa mbabe wa zamani wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba, wakati huu waendesha mashtaka wakitoa kiwango cha chini cha adhabu kutopungua miaka 25.

Jean Pierre Bemba Makamu wa rais wa zamani wa DRC
Jean Pierre Bemba Makamu wa rais wa zamani wa DRC AFP/MICHAEL KOOREN
Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashtaka wamemlaumu Makamu wa rais wa zamani wa DRC kufumbia macho ukatili uliofanywa na majeshi yake nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati mnamo October 2002 hadi Mei 2003.

Bemba alipatikana na hatia mnamo mwezi Machi kwa mashtaka matano ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu baada ya kutuma kikosi chake kilichokuwa na wanajeshi elfu moja na mia tano nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati kwenda kusaidia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya raisi aliyekuwepo madarakani kipindi hicho.

Kikosi cha (MLC) chini ya uongozi wa Bemba kilitekeleza mfululizo wa matukio ya ubakaji na mauaji wakati wakitafuta kumpindua rais wa wakati huo Ange-Felix Patasse.

Wataalam wanaeleza kuwa ukatili wa matukio hayo utakuwa na madhara ya muda mrefu kwa waathirika na jamii zao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.