Pata taarifa kuu
UN-ERITREA

UN yailaumu Eritrea kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu

Umoja wa Mataifa unasema serikali ya Eritrea imetekeleza makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu tangu ilipopata uhuru mwaka 1991.

Mji wa Eritrea, Asmara.
Mji wa Eritrea, Asmara. © REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja huo iliyochunguza mateso na namna mauji yalivyotokea nchini humo inasema serikali ya Eritrea imesababisna vifo vya maelfu ya watu na wengine wameteswa.

Mike Smith aliyeongoza uchunguzi huo amesema rais Isaias Afwerki anahusika moja mwa moja na anastahili kushatakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC.

Raia wa Eritrea wamekuwa wakikimbia nchi yao kwa madai ya kuhofia kuuawa au kuteswa na vikosi vya serikali.

Serikali ya Eritrea imekanusha tuhma hizo za Tume ya Umoja wa Mataifa na kusema ni za uongo na hazina msingi wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.