Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Misri: wafungwa 6 wahukumiwa kifungo cha miaka 7 jela

Wafungwa sita wamehukumiwa Jumapili hii kifungo cha miaka saba gerezani nchini Misri wakituhumiwa kumpiga hadi kufa raia mmoja wa Ufaransa mwaka 2013 aliyekuwa kizuizini, katika kituo cha polisi.

Polisi ya Misri ikiwa kwenye eneo kulikotokea shambulio mbele ya chuo kikuu cha Cairo, Oktoba 22 mwaka 2014.
Polisi ya Misri ikiwa kwenye eneo kulikotokea shambulio mbele ya chuo kikuu cha Cairo, Oktoba 22 mwaka 2014. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo familia za watuhumiwa hao na upande wa utetezi wameishtumu polisi kuhusika na kifo cha raia huyo wa Ufaransa.

Eric Lang, mwenye umri wa miaka 49, ambaye alikua akifundisha Kifaransa nchini Misri, alikufa baada ya kupigwa vibaya Septemba 13, 2013. Alikua alizuiliwa kwa wiki moja katika kituo cha polisi mji Cairo baada ya kukamatwa katika mtaa mmoja kwa sababu alikua hana kitambulisho na pasi yake ya kusafiria, iliyopelekwa baadaye kwa askari polisi, haikuwa na viza vya kuishi nchini Misri, kwa mujibu wa mamlaka ya Misri.

Kulingana na hati ya mashtaka, Eric lang alipigwa na wafungwa sita wenzake katika sehemu alipokua akizuiliwa. Wafungwa hawa sita wamepatikana na hatia ya "kipigo kiliyosababisha kifo" Jumapili hii na mahakama ya mjini Cairo, kwa mujibu wa uamuzi uliyosoma na karani. Wamehukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani.

Wanasheria wa watuhumiwa, ambao wanatarajia kukata rufaa, wamelaani toleo la hati ya mashtaka, wakidai kuwa uchunguzi wa madaktari ulionyesha kuwa Eric Lang alipigwa chuma na waya ya umeme hadi kufa, huku wakibaini kwamba mauaji yanaweza tu kuwa yalitekelezwa na askari polisi au kwa njama na ridhaa yao.

Mama na dada wa Eric Lang, pia, wamesema wana mashaka na toleo la serikali. Wamefungua mashitaka dhidi makamishina wawili wa polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani hasa kwa "kumzuia mtu" na "kutowajibika kumuokoa katika hatari".

Polisi ya Misri mara kwa mara inatuhumiwa na mashirika ya kimataifa na yale ya Misri ya kutetea haki za binadamu kuhusika na kuwatesa na kuwaua wafungwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.