Pata taarifa kuu
ALGERIA-BOUTEFLIKA

Algeria: Rais Bouteflika yuko Geneva kwa matibabu

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, anaedhoofika kwa matatizo ya kiafya, amejielekeza Jumapili hii mjini Geneva kufanyiwa uchunguzi wa afya "ambayo inazorota kila mara", Ofisi ya rais wa Algeria imetangaza.

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika wakati wa kuapishwa kwa muhula wake wa nne, Aprili 28 mwaka 2014.
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika wakati wa kuapishwa kwa muhula wake wa nne, Aprili 28 mwaka 2014. REUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Bw Bouteflika, ambaye ana umri wa miaka 79, alishikwa mwaka 2013 na kiharusi, maradhi ambayo yalimdhoofisha uwezo wake wa kukaa na kufanya kila shughuli atakavyo. Tangu wakati huo anatumia kiti cha walemavu na anafanya kazi makazi yake mjini Zeralda, Magharibi mwa mji mkuu wa Algiers, ambapo anapokea hasa wageni kutoka nje.

Bw Bouteflika amejielekeza "Jumapili Aprili 24, 2016 mjini Geneva, kwa ziara ya kibinafsi, wakati ambapo atafanyiwa uchunguzi wa afya anaofanyiwa baada mara kwa mara," Ofisi ya rais imebainisha katika taarifa yake.

Hali ya afya ya rais wa Algeriaimekua ni gumzo nchini humo, huku uvumi umekua ukizagaa, baada ya picha iliyorushwa hewani Aprili 10, ambapo alionekana mdhaifu kabisa.

Maneno aliyoandika Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, kuhusu picha hiyo, yalishtumiwa na watu wa karibu wa Bw Bouteflika, na kuzua hali ya sintofahamu katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Bw Valls alionekana ni mwenye hatia wa "utovu wa nidhamu" na "uovu," Baraza la Taifa (Seneti) lilisema Alhamisi Aprili 21.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.