Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-CHIBOK

Nigeria: miaka 2 tangu wasichana wa Chibok kutekwa nyara

Alhamisi hii, Aprili 14 inaadhimishwa miaka miwili ya utekaji nyara wa wasichana 276 wanafunzi wa shule ya Chibok, ambao walitekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Boko Haram kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Maandamano ya watu kutoka familia za wasichana wanafunzi wa shule ya Chibok waliotekwa nyara na Boko Haram, miaka miwili iliyopita, Nigeria.
Maandamano ya watu kutoka familia za wasichana wanafunzi wa shule ya Chibok waliotekwa nyara na Boko Haram, miaka miwili iliyopita, Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Tangu wakati huo, kundi, ambalo lilijiita Islamic State Afrika Magharibi, liliwateka nyara mamia ya wasichana wengine, ikiwa ni pamoja na karibu 400 katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka 2014 katika kijiji cha Damasak, kusini mwa mpaka wa Niger.

Kwa sasa vijana wengi hasa wasichana wako mikononi mwa magaidi waliodhoofika kijeshi kwa mwaka mmoja sasa, na wanatumia kama ngao.

Wasichana hawa walizuiliwa wakati fulani katika mji wa Gwoza, mji uliochaguliwa na Boko Haram mwezi Agosti 2014 kama mji mkuu wa mkuu wa kundi hili. Jeshi la Nigeria ililiendesha mashambulizi katika mji huo na kwatimua wanamgambo wa Boko Haram, lakini inaonekana kwamba wapiganaji hawa waliondoka na wasichana hawa katika msafara wao.

Baadhi ya wasichana waliofaulu kutoroka wameelezea masaibu wyalio wakuta. Wanabaini kwamba walifanyiwa mateso mengi.

Ni miaka miwili sasa tangu wasicahana 267 wa shule ya Chibok kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Boko Haram. Mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu waliko wasichana hao.

Wengi wanadhani labda wako Chad ama Cameroon. Lakini wadadisi wanabaini kwamba kuna uwezekano mkubwa wengi wao walilazimishwa kuolewa na wapiganaji. Mpaka sasa wasichana 200 hawajapatikana hadi leo.

Hata hivyo maisha yanaendelea kurejea taratibu katika hali ya kawaida mjini Chibok na usalama umeanza kuimarika.

Watu wamekua wakijiuliza : inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?

Kitendo hiki cha Boko Haram cha kuwateka nyara wasichana hawa kililaaniwa vikali kimataifa na kuchochea kampeni ya mitandao ya kijamii iliyojulikana kama "bringbackourgirls" na kuweka wazi udhalimu unaotekelezwa na makundi ya uasi kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.