Pata taarifa kuu
RDC-EDEM KODJO-MAZUNGUMZO-SIASA

Edem Kodjo: kuanza kwa mazungumzo wiki hii DRC

Msuluhishi wa mazungumzo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Edem Kodjo, ametangaza Jumatatu hii Aprili 11 kuwa ameitisha mazungumzo ifikapo mwishoni mwa wiki hii.

Msuluhishi wa mazungumzo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Edem Kodjo.
Msuluhishi wa mazungumzo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Edem Kodjo. © Gallimard
Matangazo ya kibiashara

Edem Kodjo alikutana na waandishi wa habari mjini Kinshasa. Atateua kwanza kamati ya maandalizi kabla ya mazungumzo maalumu.

Tangu mwanzo, Edem Kodjo alionyesha matumaini yake. Katibu Mkuu wa zamani wa OAU ametangaza kuanza kwa mazungumzo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yatakayowashirikisha wadau wote ifikapo mwishoni mwa wiki hii. "Hakuna kisichowezekani kwa watu wenye nia njema. Wiki hii, ninapanga kuweka kamati ya maandalizi, " Edem Kodjo ametangaza.

Je, mazungumzo haya yatachukua muda gani? Edem Kodjo mwenyewe bado hajajua. Hata hivyo, Msuluhishi ametangaza kuanza na wale ambao watakua tayari kushiriki mazungumzo hayo. Mlango utabaki wazi na wengine wanaweza kujiunga wakati mazungumzo hayo yakiendelea.

Muungano wa vyama vikuu saba bado vinakataa kushiriki

Hata hivyo, chama kikuu kongwe cha upinzani cha UDPS kiko tayari kushiriki katika mazungumzo hayo yatakayoongozwa na Edem Kodjo. "Leo hii katika upinzani ninaungwa mkono na chama cha UDPS na mimi nachukua fursa hii kumshukuru Kiongozi wa chama hicho Etienne Tshisekedi na wasaidizi wake kwa kuruhusu kufanyika kwa mazungumzo hayo," Edem Kodjo amesema. Licha ya maneno haya, chama cha UDPS bado kina wasiwasi kuhusu uteuzi wa Edem Kodjo kuwa mpatanishi katika mazungumzo hayo. Chama cha Etienne Tshisekedi hakipingi mazungumzo, lakini msemaji wake yuko wazi kabisa: vyama vinapaswa, hadi Aprili 24, kujikubalisha kuhesimu Katiba ya nchi.

"Ni lazima yote hayo yafanyike kwa mujibu wa katiba. Hatuwezi kwenda zaidi ya muda uliopangwa kikatiba. Hatuwezi kukubali kwenda uchaguzi katika mazingira tuliomo sasa," Augustin Kabuya amesema.

Muungano wa vyma vikuu saba vya upinzani (G7) mpaka sasa haujabadili msimamo wake. Muungano huu umeendelea kusisitiza kwamba hautashiriki katika mazungumzo hayo, ukibaini kwamba mazungumzo hayo yaliitishwa na Joseph Kabila, kupitia Edem Kodjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.