Pata taarifa kuu
MISRI-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Moja kati ya mikataba kati ya Misri na Saudi Arabia waibua mgawanyiko

Miongoni mwa mikataba mingi iliyosainiwa mwishoni mwa wiki hii kati ya Riyadh na Cairo, mmoja wao umezua utata mkubwa nchini Misri. Mkataba huo unahusu visiwa viwili vya bahari ya Sham vya Tiran na Sanafir.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi (kushoto) pamoja na Mfalme Salman wa Saudi Arabia, Aprili 7, 2016 Cairo, Misri.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi (kushoto) pamoja na Mfalme Salman wa Saudi Arabia, Aprili 7, 2016 Cairo, Misri. REUTERS/Saudi Press Agency
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mikataba mingi iliyosainiwa mwishoni mwa wiki hii kati ya Riyadh na Cairo, mmoja wao umezua utata mkubwa nchini Misri. Mkataba huo unahusu visiwa viwili vya bahari ya Sham vya Tiran na Sanafir.

Visiwa hivi vilikua chini ya milki ya Misri, lakini kuanzia mwishoni mwa wiki hii viko chini ya milki ya Saudi Arabia. Ni katika visiwa hivyo ambapo kutajengwa daraja litakalo unganisha nchi hizi mbili.

Mfalme Salman wa Saudi Arabia alipokelewa Jumapili 10 Aprili, kwa shangwe na nderemo katika Bunge la Misri. Rais wa Misri Abdel Fatah Al Sissi alitoa hotuba chini ya vifijo vya Wabunge ambao wameonekana wakipuuzia hali ya sintofahamu inayoigawa nchi ya Misri kwa sasa.

Ni katika kisiwa cha Tiran na Sanafir ambapo kutajengwa daraja litakalo unganisha Misri na Saudi Arabia. Kwa sasa hali ya sintofahamu imeibuka kufuatia mkataba huo unaoikabidhi Saudi Arabia visiwa hivyo viwili viliokua chini ya milki ya Misri. Kisiwa cha Sanafir na Tiran hasa vinadhibiti barabara inayoelekea Ghuba ya Akaba na bandari ya Israel ya Eilat na ile ya Jordan ya Akaba. Uamuzi wa Nasser wa kufunga barabara ya Tiran ulisababisha vita vya 1967 pamoja na Israel ambavyo ilividhibiti hadi mkataba wa amani na Cairo.

Leo Tiran inashikiliwa na kikosi cha kimataifa na Wachunguzi wa eneo la Sinai. Miongoni mwa mikataba iliyosainiwa wakati wa ziara ya Mfalme Salman nchini Misri, mmoja wao unaweka mipaka ya baharini na inaweka visiwa viwili katika maeneo ya majini ya Saudi Arabia. Ryad iliiomba Misri mwaka 1950 "kuhakikisha usalama wa visiwa hivyo viwili," serikali ya Misri imejieleza katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.