Tanzania yanyimwa dola 472 kufuatia uchaguzi Zanzibar
Shirika la Marekani linalohusika na malengo ya Milenia limesema limesitisha msaada wake wa Dola Milioni 472 kwa serikali ya Tanzania, kutokana na marudio ya uchaguzi Visiwani Zanzibar.
Imechapishwa:
Fedha hizo zilinuiwa kuisadia serikali ya Tanzania kuunganisha umeme kwa raia wake wa vijijini.
Waziri wa Mambo ya nje wa Tanznaia Augustine Mahiga amesema ameshangazwa na hatua hiyo na kusema shirika hilo halikuzingatia juhudi za demokrasia zilizopigwa nchini Tanzania.
Marekani na Mataifa ya Ulaya, yalipinga kufanyika kwa marudio ya uchaguzi uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani CUF kwa kile ilichosema kuwa uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa huru na halali.