Pata taarifa kuu
MISRI-USAFIRI-UTEKAJI NYARA

EgyptAir yatekwa nyara: abiria atishia kulipua mkanda wake

Ndege ya shirika la ndege la Misri EgyptAir iliyokuwa imebeba abiria 81 na wafanyakazi 7 ikifanya safari kati ya Alexandria na Cairo ambayo ilikua imetekwa nyara na watu wasiojulikana imetua katika mji wa Larnaca, nchini Cyprus.

Ndege ya shirika la ndege la Misri EgyptAir kwenye lami ya uwanja wa ndege wa Larnaca, Cyprus, Machi 29, 2016.
Ndege ya shirika la ndege la Misri EgyptAir kwenye lami ya uwanja wa ndege wa Larnaca, Cyprus, Machi 29, 2016. REUTERS/Yiannis Kourtoglou
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii ni kwa mujibu wa runinga ya serikali ya Cypus na mamlaka ya uwanja wa ndege wa Cairo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, abiria wa Misri

wanasadikiwa kuwa wameondolewa katika ndege hiyo mjini Larnaca.

Shirika la habari la Ufaransa la AFP limebaini kwamba abiria ametishia kulipua mkanda wake kwa mujibu wa vyanzo vya mamlaka ya usafiri wa anga.

Watekaji nyara waliwasiliana na maafisa mamalaka ya uwanja wa ndege saa 8:30 asubuhi saa za Cyprus (sawa na saa 5:30 asubuhi alfajiri saa za kimataifa) na ndege hiyo aina ya Boeing 737-800, ambayo ilikuwa ikifanya safari kati ya Alexandria na Cairo ilipewa kibali cha kutua saa 8:50 asubuhi, polisi imesema.

Watekaji nyara hawajazungumza chochote na kikosi cha askari polisi kimetumwa katika uwanja wa ndege wa Larnaca.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.