Pata taarifa kuu
TUNISIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Tunisia: mapigano mapya yatokea Ben Guerdane

Wanajihadi wawili na askari mmoja wameuawa katika mapigano mapya yaliotokea katikamkoa wa Ben Guerdane, kusini mashariki mwa Tunisia karibu na nchi ya Libya, ambako maelfu ya watu waliwazika Jumatano hii wahanga wa mashambulizi yaliopita.

Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid, Machi 8, 2016.
Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid, Machi 8, 2016. FATHI NASRI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mashambulizi yalioendeshwa Jumatatu wiki hii dhidi ya kambi ya kijeshi, kituo cha polisi na kituo kimoja cha kikosi cha Walinzi wa Taifa katika moa wa Ben Guerdane, "magaidi" 46 kwa jumla wameuawa, pamoja na askari polisi 12 na raia saba, kwa mujibu wa vyanzo rasmi.

Hakuna kundi hata moja mpaka sasa, limedai kuendesha mashambulizi haya lakini mamlaka ya Tunisia inalinyooshea kidole cha lawama kundi la Islamic State (IS) kwamaba linajaribu kuweka "ngome yao kuu" katika mkoa wa Ben Guerdane, karibu na Libya, nchi ambayo imetumbukia katika machafuko na ambapo kundi hili la IS linaendesha harakati zake.

Tangu mapinduzi ya mwaka 2011, Tunisia inakabiliwa na kuongezeka kwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu ambayo yanahusika kwa vifo kadhaa ya askari polisi na wanajeshi pamoja na watalii, lakini mashambulizi yaliotokea wakati mmoja Jumatatu katika mkoa wa Ben Guerdane ni mabaya kabisa kuwahi kutokea tangu mwanzoni mwa mwaka huu nchini humo.

Jumanne jioni na Jumatano hii, wanajihadi 10 wameuawa Ben Guerdane, mji wenye wakazi 60,000 ambao umewekwa chini ya amri ya kutotoka nje usiku tangu Jumatatu wiki hii.

Jumanne usiku, jeshi na vikosi vya usalama wamewaua wanajihadi saba ambao walikua walikimbilia katika nyumba moja mjini Ben Guerdane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.