Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAUAJI-USALAMA

Burundi: maswali mengi kuhusu kaburi la halaiki la Mutakura

Wakati ambapo wataalam watatu waliotumwa na Umoja wa Mataifa wakiendelea na mazungumzo yao mjini Bujumbura, vita vya maneno na mawasiliano vimeendelea nchini Burundi.

Watu wakiwa karibu ya mwili wa mmoja wa watu sita waliouawa Julai 1 wakati wa operesheni ya awali ya polisi ya Burundi mjini Bujumbura katika kata ya Mutakura.
Watu wakiwa karibu ya mwili wa mmoja wa watu sita waliouawa Julai 1 wakati wa operesheni ya awali ya polisi ya Burundi mjini Bujumbura katika kata ya Mutakura. AFP PHOTO / MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Wiki hii, serikali ya Bujumbura ilionyesha kaburi la halaiki lililogunduliwa katika moja ya kata kulikofanyika maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza ya Mutakura. Kama mifupa ya miili ya watu watatu tu ilitolewa kaburini, serikali inadai kuwa watu 30 walizikwa katika kaburi hilo, huku ikishtumu waandamanaji dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza kuhusika na mauaji hayo. Serikali ilitaja idadi ya watu thelathini waliozikwa katika kaburi hilo, wakati ambapo kulionekana miili mitatu pekee.

Watu waliouawa na kuzikwa katika kaburi hilo wanasadikiwa kuwa wafuasi wa chama madarakani cha CNDD-FDD, hasa vijana wakereketwa wa chama hicho Imbonerakure (vuguvugu la vijana wa chama tawala), kwa mujibu wa Meya wa jiji la Bujumbura. Lakini katika hotuba hii, upinzani na mashirika ya kiraia yameonyesha maeneo kadhaa ambako kunadaiwa kuwa walizikwa kwa pamoja watu waliouawa kutokana na msimamo wao wa kupinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati huru ya taifa ya haki za binadamu nchini Burundi (CNIDH) ametufautisha kauli hizi. Wakati huo huo chama tawala, katika tangazo lake, kimezungumzia kuhusu kugunduliwa kwa kaburi hili katika kata ya Mutakura, kikinyooshea kidole vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia, kwa mujibu wa chama hicho viliochochea vurugu, vikidai kupinga muhula wa tatu wa Rais Nkurunziza.

Zoezi la kukua kaburi hili lingeliendelea Jumanne wiki hii, lakini lilisimamishwa. "Tunatoa nafasi kwa wataalam wenye uzoefu ili kuamua kama kaburi hili ni la hivi karibuni au la," Jean-Baptiste Baribonekeza, Mwenyekiti wa CNIDH amesema.

Baribonekeza amesema ni mapema mno kuzungumzia kuhusu tarehe, mazingira au waliohusika na mauaji ya watu hao watatu. "Wanaweza kuwa watu walio karibu na serikali, au raia wa kawaida," Baribonekeza ameongeza.

Kauli ya serikali bado haijathibitishwa lakini inaeleza kufuatia mtu ambaye inadaiwa kuwa alikiri mwenyewe kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa gazeti la Iwacu, miili hiyo iliotolewa katika kaburi hilo la Mutakura ilikua na alama za kupigwa wakati ilipoonyeshwa mbele ya vyombo vya habari.

Upinzani ulionje na mashirika ya kiraia vimetupilia mbali madai hayo ya serikali na kubaini kwamba hiyo ni mbinu ya serikali ya kutaka kukwepa tuhuma dhidi yake.

Itafahamika, mwezi Desemba mwaka 2015, serikali ilifutilia mbali ombi la Umoja wa Mataifa la kutuma wataalam wake nchini Burundi ili kuendesha uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na madai ya makaburi ya halaiki 9 yalioelezwa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Human Right Watch, Amnesty International na mengineyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.