Pata taarifa kuu
NIGER-UCHAGUZI-SIASA

Niger: uchaguzi mkuu wafanyika Jumapili

Raia milioni 7.5 wa Niger wamepiga kura Jumapili hii kwa kumchagua rais wao. Naye Rais anayemaliza muda wake Mahamadou Issoufou anagombea muhula wa pili wa miaka mitano dhidi ya upinzani unaolalamikia uchaguzi kugubikwa na udanganyifu baada ya kampeni iliokua iligubikwa na hali tete.

Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou anayemaliza muda wake katika mji wa Niamey, Februari 18, 2016.
Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou anayemaliza muda wake katika mji wa Niamey, Februari 18, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kupiga kura lilichelewa saa moja kutokana na ukosefu wa vifaa vya uchaguzi au kutokuwepo kwa maafisa wa vituo vy kupigia kura.

Vituo 25,000 vya kupigia kura vitafungua saa mbili saa za Niger na kufungwa karibu saa moja usiku katika nchi hii ya wakazi milioni 19 ambayo ni miongoni mwa nchi maskini duniani na inayokabiliwa na tishio la makundi ya kiislamu ikiwa ni pamoja na kundi la Boko Haram.

Hata hivyo eneo la Diffa (Kusini-Mashariki) linalokabiliwa na mashambulizi ya kundi la Boko Haram, vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa kumi na moja asubuhi saa za Niger na vitafungwa saa kumi na moja jioni kwa sababu ya utofauti wa mwangaza.

"Vikosi vya usalama vinapiga doria vikitumia magari 1,000 kwa masaa 24 kwa 24 nchi nzima yenye ukubwa wa (kilomita mraba milioni 1.3) ikiwa ni pamoja na gari moja angalau kwa vijiji 25," Waziri wa Mambo ya Ndani, Hassoumi Massaoudou alisema kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza.

Uchaguzi huu wa urais umefanyika sambamba na ule wa wabunge na matokeo yatatangazwa ndani ya siku tano baada ya uchaguzi.

Rais Issoufou, mwenye umri wa miaka 63, kwa jina maarufu la "simba", ametangaza ushindi kwa "asilimia kubwa" katika duru ya kwanza ya uchaguzi, wakati ambapo upinzani ambao umegawanyika, umeahidi kuungana katika dudu ya pili.

Upinzani unamtuhumu Rais Issoufou kuandaa "wizi wa kura" katika uchaguzi huu. Hofu ya machafuko ya baada ya uchaguzi imeanza kutanda.

"Kama Issoufou atashinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi, atakua ameiba. Wakati huo, tutasusia shughuli zote (kufanya mgomo) na kutakuwa na mapigano," mfuasi wa Hama Amadou, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema. Hama Amadou anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo aambapo wanashiriki wagombea 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.