Pata taarifa kuu
LIBYA-SERIKALI YA UMOJA

Libya: Uundwaji wa serikali ya umoja wakabiliwa na hofu ya kupitishwa

Baada ya wiki yenye utata, serikali ya umoja wa kitaifa hatimaye imetangazwa nchini Libya, lakini kupitishwa kwake kumejawa na wasiwasi na Bunge linalotambuliwa kimataifa, ambalo limeahirisha kuwa zoezi hili litafanyika Jumanne hii.

Waziri Mkuu mteule wa Libya, Fayez el-Sarraj (kushoto), Februari 15, 2016 katika mji wa Skhirat, Morocco.
Waziri Mkuu mteule wa Libya, Fayez el-Sarraj (kushoto), Februari 15, 2016 katika mji wa Skhirat, Morocco. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Martin Kobler, ametoa wito kwa Bunge mjini Tobruk (Mashariki) kutoacha "fursa hii ya kipekee" ili kuondoa nchi ya Libya katika machafuko yanayodumu tangu kuanguka kwa utawala wa dikteta Gaddafi.

Wabunge wamekutana Jumatatu hii mchana, lakini kikao kilisimamishwa mara moja na kuahirishwa hadi Jumanne wiki hii.

Kabla ya kupitishwa au la kwa serikali mpya yenye mawaziri 18, wabunge wanataka "kujua kuhusu mpango wa serikali hiyo na kujadili mlolongo wa shahada za masomo na kazi walizozifanya Mawaziri hao", Khalifa al-Deghari, mmoja wa Wawabunge waliokuwepo katika kikao hicho, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP moja ya manaibu sasa, Khalifa al-Deghari.

Mapema usiku wa manane, orodha ya mawaziri ilikuwa imetolewa na Baraza la Rais. Serikali hiyo inaundwa na mawaziri 28 ikiwa ni pamoja na wajumbe tisa kutoka upande unaopinga serikali inayotambuliwa kimataifa na kuongozwa na Waziri Mkuu mteule Fayez al-Sarraj. Maafisa hao walikua wamekusanyika kwa siku kadhaa katika mji wa Skhirat nchini Morocco ambapo kunafanyika mazungumzo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.

"Ni matumaini yetu kwamba serikali hii itaonyesha mwanzo na mwisho wa migogoro nchini Libya", msemaji wa Baraza la Rais, Fathi al-Mejebri amesema.

Tangazo hilo limekuja dakika chache kabla ya tarehe ya mwisho iliotolewa na Bunge linalotambuliwa kimataifa kwa ajili ya kuwasilisha serikali mpya. Orodha ya kwanza ambayo ilikuwa na wajumbe 32 ilifutiliwa mbali tarehe 25 Januari, idadi ya wajumbe hao ilionekana kuwa ni kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.