Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-KENYA-ICC

Viongozi wa Afrika waonesha kuunga mkono azimio la Kenya kutaka nchi hizo zijitoe kwenye mkataba wa Roma

Nchi ya Kenya imeendelea na harakati zake za kuwashawishi viongozi wa Afrika kuunga mkono mapendekezo yake ya kujiondoa kwenye mkataba wa Roma unaoitambua mahakama ya kimataifa ya ICC.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mkutani wa 26 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliokuwa unafanyika mjini Addis Ababa, rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliendelea na juhudi za Serikali yake kuwataka viongozi wenzake kuunga mkono harakati za kujiondoa kwenye mkataba wa Roma.

Rais Kenyatta amesema kuwa ni wazi mahakama hiyo inafanya kazi zake kisiasa, na kwamba inashinikizwa na baadhi ya nchi za magharibi kutekeleza majukumu yake, majukumu ambayo anasema yanawalenga zaidi viongozi wa Afrika.

Mapendekezo haya ya Serikali ya Kenya yalionekana kuungwa mkono karibu na viongozi wote wa Umoja huo, ambao walikubaliana kuujadili na kuupitisha katika mkutano ujao, ambapo ikiwa utapitishwa, basi nchi zote wanachama za Umoja wa Afrika zitajiondoa kwa pamoja kwenye mahakama hiyo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Nairobi, Julai 21 mwaka 2015.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Nairobi, Julai 21 mwaka 2015. REUTERS/Noor Khamis

Mapendekezo haya ya Kenyatta, anayawasilisha ikiwa ni miezi kadhaa imepita toka ujumbe wa nchi yake ushindwe kuwashawsihi nchi wanachama zinazounda mkataba wa ICC, ambazo zilikataa kufutwa kwa kesi dhidi ya viongozi wa Kenya.

Licha ya mapendekezo haya, tayari viongozi wengi wa Afrika ikiwemo nchi ya Uganda, zimeunga mkono kujitoa kwenye mkataba huo, huku katika mikutano iliyopita ya wakuu wa nch waliridhia kutoshirikiana na mahakama hiyo.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa licha ya mapungufu yaliyopo kwenye mahakama hiyo, haitoshi kwa nchi hizo kujiondoa na kuhoji ni kwanini viongozi wa Afrika wanahisi wao ndio walengwa wakuu wa mahakam hiyo.

Suala hili limeletwa tena na nchi ya Kenya, wakati huu kesi dhidi ya naibu wa rais William Ruto ikiendelea kwenye mahakama hiyo, huku pia kesi dhidi ya rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo nayo ikiwa imeanza kusikilizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.