Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-MAUAJI

Nigeria: watu 13 wameuawa katika mashambulizi ya kujitoa mhanga Chibok

Washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga wamejilipua Jumatano hii, na kuua watu wasiopungua 13 katika mji wa Chibok, kaskazini mwa Nigeria, ambapo kundi la kiislam la Boko Haram liliwateka nyara zaidi ya wanafunzi 200 wa shule ya sekondari mwaka 2014, viongozi wa mji huo wamesema.

Mwanamke huyu akipita mbele ya shule ya Chibok Aprili 14, 2015.
Mwanamke huyu akipita mbele ya shule ya Chibok Aprili 14, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi, ambayo yalitokea karibu saa sita mchana (sawa na saa 5:00 mchana saa za kimataifa), yamelenga soko, kiongozi mmoja, Ayuba Chibok, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Watu kumi wameuawa katika maeneo ya mashambulizi, mwingine alifariki wakati alipokua akipelekwa hospitali na wengine wawili, mwanamke na mtoto, wamefariki kutokana na majeraha waliyoyapata wakati ambapo walikua wametibiwa, Dazzban Buba, aliyekuwepo hospitali ya mji wa Chibok amebaini.

watu thelathini wengine wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na 21 ambao wamejeruhiwa vikali, na tisa wameruhusiwa baada ya kupata matibabu, Dazzban Buba amesema. Waathirika wengi wanauguza majeraha yaliyotokana na milipuko hiyo.

Kwa uchache watu 32 waliuawa Jumatatu katika mashambulizi matatu ya kujitoa mhanga katika soko la kijiji, kaskazini mwa Cameroon. Lilikua shambulio la tatu katika eneo hilo tangu mwanzoni mwa mwaka huu, shambulio ambalo lilihusishwa kundi la Boko Haram, ambalo pia liliendesha mashambulizi mara tatu nchini Nigeria tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na kuua watu kumi na tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.