Pata taarifa kuu
ICC-ONGWEN

ICC yachunguza ushahidi kuhusu kesi dhidi ya Dominic Ongwen

Kwa miaka mingi, Dominic Ongwen alikuwa mmoja wa viongozi wa kuu wa kundi la waasi wa Uganda la LRA na alitekeleza na kundi hilo mauaji dhidi ya raia katika nchi yake, lakini pia nchini Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Dominic Ongwen, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Uganda la LRA, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague, wakati wa ukisikilizwa uthibitisho wa mashitaka, Januari 21, 2016.
Dominic Ongwen, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Uganda la LRA, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague, wakati wa ukisikilizwa uthibitisho wa mashitaka, Januari 21, 2016. © REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Uthibitisho wa tuhuma zinazomkabili uliyoanza Alhamisi iliyopita, utaendelea kusikilizwa Jumatatu hii. Lengo kwa mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa: kuwashawishi majaji kushikilia kesi hiyo.

Uthibitisho wa mashtaka unadumu siku tano kwa jumla. Lengo kwa Mahakama ya Kimataifa ni kuhakikisha kuwa ushahidi dhidi yaDominic Ongwen ni wa kutosha kwa kushikilia kesi hiyo. Kuanzia Jumatatu, wanasheria watawasilisha waathirika zaidi ya 2,000, ambao waliotoa ushahidi wa mauaji yanayoshukiwa kuetekelezwa na kundi la waasi wa Uganda la LRA.

Akichukulia katika harakati zao za zamani lakini pia video au sauti ziliyorekodiwa, mwendesha mashitaka ametoa orodha ya mashtaka 70 ya vitendo viliyotekelezwa kati ya mwaka 2002 na 2005: uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mateso, uporaji, utumwa .

Dominic Ongwen, alietekwa na wapiganaji wa LRA wakati alipokua mtoto, pia alishiriki katika utekaji nyara wa vijana. Wavulana walikuwa wakilazimishwa kupigana, wasichana kubakwa na kulazimishwa kuolewa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda la LRA.

Mashitaka 70

Mahakamani, Dominic Ongwen alizungumza maneno machache kwa lugha yake ya Atcholi, alipoulizwa kuthibitisha kwamba anafahamu mashtaka yanayomkabili. Muda wote uliofuata alisalia kimya, alionekana akizungusha ulimi kinywani, bial hata hvyo kusema neno lolote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.