Pata taarifa kuu
TUNISIA-MAANDAMANO-VURUGU

Tunisia yatangaza amri ya kutotoka nje usiku

Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa nchini kote Tunisia Ijumaa hii, baada ya siku nyingi za maandamano ya kipekee ya kijamii kwa ukubwa wake na muda wake tangu mapinduzi ya mwaka 2011.

Askari polisi wa Tunisia wakichunguza maandamano katika mji waTunis, Januari 18, 2016.
Askari polisi wa Tunisia wakichunguza maandamano katika mji waTunis, Januari 18, 2016. MOHAMED KHALIL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Miaka mitano baada ya kuangushwa kwa utawala wa Zine El Abidine Ben Ali, maandamano dhidi ya umaskini na haki kwa kijamii yalianza katika jimbo la watu wasiojiweza wa Kasserine (katikati mwa nchi) kufuatia kifo Jumamosi cha kijana ambaye hakua na ajira.

Maandamano haya yalisamba siku za karibuni katika miji mingine mingi na yaligubikwa Alhamisi hii hasa na vurugu katikaeneo la Grand Tunis.

Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 11:00 alfajiri (sawa na saa 1:00 usiku hadi 10:00 alfajiri saa za kimataifa) "kufuatia mashambulizi dhidi ya mali za umma na za watu binafsi na kwamba muendelezo wa vitendohivyo ni kama hatari kwa usalama wa nchi na wananchi", kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Hatua hiyo kama hiyo iliwahi kuchukuliwa jioni wakati wa shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya kikosi cha usalama wa rais (lililowaua maafisa 12) lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS) Novemba 24 mjini Tunis.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.