Pata taarifa kuu
MOROCCO-UFARANSA-UGAIDI

Morocco yamkamata raia wa Ubelgiji mhusika wa mashambulizi ya Paris

Mamlaka ya Morocco imetangaza Jumatatu hii kwamba imemkamatwa raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco ambaye alihusika "moja kwa moja" katika mashambulizi ya Novemb ya jijini Paris , wakati ambapo uchunguzi wa mashambulizi hayo umeendelea Ubelgiji.

Le Carillon, katika wilaya ya 10 ya jijini Paris, ni moja ya baa zilizolengwa na mashambulizi, Novemba 13, 2015,  ilifungua milango yake Januari 13.
Le Carillon, katika wilaya ya 10 ya jijini Paris, ni moja ya baa zilizolengwa na mashambulizi, Novemba 13, 2015, ilifungua milango yake Januari 13. © REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ubelgiji, aliyetambuliwa tu herufi za mwanzo za majina yake, alikamatwa Januari 15 katika mji wa al-Mohammadiya karibu na mji waCasablanca, Wizara ya Mambo ya Ndani mjini Rabat imesema katika taarifa yake.

Anahusika moja kwa moja katika mashambulizi yaliyotokea jijini Paris G.A" yaiyosababisha vifo vya watu 130 Novemba 13. Mashambulizi ambayo yalidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS), taarifa hiyo imeongeza.

Kwa mujibu wa mtandao wa Morocco wa habari Le360, ulio karibu na Kasri la kifalme, mtu aliekamatwa alikamatwa katika nyumba ya mama yake akiwa peke yake. Mama yake kwa sasa yuko Ubelgiji na baba yake alifariki. Mtu huyo baadaye alitambuliwa kama Gelel Attar, mwenye umri wa miaka 26, Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imebaini.

Kwa mujibu wa utafiti wa Morocco, raia huyo wa Ubelgiji alikutana nchini Syria na Abdelhamid Abaaoud mshukiwa anayetuhumiwa kuandaa mashambulizi yaliyoendeshwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris Novemba 13. Alijiunga mara ya kwanza na kundi la Al-Nosra Front, tawi la la Al Qaeda nchini Syria kabla ya kusajiliwa na kundi la IS, wizara ya Mambo ya ya Ndani imeongeza.

Pia kwa mujibu wa utafiti wa Morocco, Attar aliondoka Syria hadi Uturuki na kisha alienda Ujerumani na Ubelgiji kabla ya kuwasili nchini Morocco akipitia Uholanzi. Mtuhumiwa huyo atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria uchunguzi utakapomalizika, imesema taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.