Pata taarifa kuu
RWANDA-ICC-SHERIA

Rwanda: Pauline Nyiramasuhuko apunguziwa kifungo

Waziri wa zamani wa Rwanda Pauline Nyiramasuhuko, aliyekuwa amepewa kifungo cha maisha kwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 amepunguziwa kifungo hicho na sasa atakuwa jela kwa miaka 47.

Hotuba ya Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika kijiji cha Nyanza, Kigali, Aprili 7, 2009.
Hotuba ya Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika kijiji cha Nyanza, Kigali, Aprili 7, 2009. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama maalum ya kimbari mjini Arusha nchini Tanzania inayomaliza kazi yake baada ya Waziri huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 69, kushinda kesi ya rufaa.

Pauline Nyiramasuhuko alipatikana na kosa hilo mwaka 2011 baada ya kuchochea mauaji hayo Kusini mwa jimbo la Butare.

Wengine waliopunguziwa vifungo vyao ni aliyekuwa Meya wa mji wa Butare Sylvain Nsabimana ambaye atakuwa jela kwa miaka 18 badala ya 25 pamoja na Joseph Kanyabashi aliyekuwa Meya wa mji wa Ngoma atakayekitumia kifungo cha miaka 20 badala ya 35.

Watu wazsiopungua laki nane wengi wao kutoka kabila la Watusti waliuawa katika nchini Rwanda mwaka 1994, baada ya ndege ya rais Juvenal Habyarimana kuangushwa katika uwanja wa ndege wa Kanombe mjini Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.