Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Mashariki ya DRC: Watu 3 wauawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama
 • Uturuki yalaani "vikali" shambulio dhidi ya msafara wa majeshi yake nchini Syria (wizara)
Afrika

Gilbert Diendéré ashitakiwa kuhusika katika mauaji ya Thomas Sankara

media Jenerali Diendéré Gilbert mkuu wa zamani wa kikosi cha usalam wa rais na mshirika wa karibu wa Blaise Compaoré. AFP PHOTO / AHMED OUOBA

Nchini Burkina Faso, jenerali Gilbert Diendéré, mkuu wa zamani wa kikosi cha usalama wa rais na mtu mwaminifu wa Rais wa zamani Blaise Compaoré, ameshtakiwa kwa akosa la "kushiriki" katika mauaji ya kapteni Thomas Sankara wakati wa mapinduzi ya Oktoba 15, 1987.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, jenerali Gilbert Diendéré ameshtakiwa kwa kosa la mauaji ya Rais Thomas Sankara. Jenerali Gilbert Diendéré anatazamiwa kueleza alichokifanya katika maandalizi na utekelezaji wa mapinduzi ya Oktoba 15, 1987, mapinduzi yaliogharimu maisha ya kapteni Thomas Sankara na washirika wake wa karibu kumi na mbili. Akithibitisha mashitaka ya mteja wake, wakili Mathieu Somé amebaini kwamba yuko tayari kuandaa utetezi wa jenerali Gilbert Diendéré.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwezi Oktoba mwaka jana, Mkuu wa Mahakama ya kijeshi alisema kuwa rais wa zamani Blaise Compaoré na mshirika wake wa karibu, jenerali Gilbert Diendéré, watafuatiliwa katika kesi ya mauaji ya kapteni Sankara mambo.

Wanasheria na familia ya Thomas Sankara bado wanasubiri matokeo ya vipimo vya DNA viliofanywa ndani ya kaburi linalokisiwa kuwa la Thoma Sankara. Uchunguzi ulionyesha kuwa mwili wa Thomas Sankara ulitobolewa na risasi alizopigwa wakati wa mapinduzi dhidi ya serikali yake. Kwa mujibu wa mwanasheria wa familia yake, rais alipigwa risasi wakati wa mapinduzi ya Oktoba 15, 1987.

Watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na askari kadhaa wa kikosi cha zamani cha usalama wa rais wameshitakiwa kwa kuhusika katika kesi hiyo. Kuhusu jenerali Gilbert Diendéré mashtaka yote hayajatangazwa rasmi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana