Pata taarifa kuu
CHINA-AFRIKA-USHIRIKIANO

Rais wa China Xi aanza ziara ya siku tano barani Afrika

Rais wa China Xi Jinping anaanza Jumanne hii Desemba 1 nchini Zimbabwe ziara ya siku tano barani Afrika, ambapo serikali za Afrika zina wasiwasi kuhusu matokeo ya kushuka kwa ukuaji wa uchumi wa China.

Rais wa China Xi Jinping akiwasili katika kikao cha mkutano kuhusu hali ya hewa Novemba 30, 2015 katika mji wa Bourget.
Rais wa China Xi Jinping akiwasili katika kikao cha mkutano kuhusu hali ya hewa Novemba 30, 2015 katika mji wa Bourget. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2009, China ni nchi ya kwanza mshirika wa Afrika, ambapo imekua ikizidisha uwekezaji na kusafirishwa kwa malighafi ya bara la Afrika ili kuhudumia raia wake.

Baada ya Zimbabwe, Xi Jinping atatembelea siku ya Jumatano mjini Johannesburg ambako atakutana na Rais Jacob Zuma kisha Ijumaa na Jumamosi atashiriki pamoja na viongozi wengine wa serikali kutoka nchi za Afrika katika mkutano wa kilele wasitakuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huu wa kilele utafanyika wakati ambapo uwekezaji wa China barani Afrika ulishuka kwa 40% katika kipindi cha kwanza cha mwaka 2015, baada ya kushuka kwa kasi kwa mahitaji ya malighafi kutoka kampuni kubwa ya Asia.

Rais Xi ataanza ziara yake mjini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe ambapo miradi ya China imekuwa nguzo kuu ya uchumi iulioendeshwa puta katika miaka kumi na tano iliyopita na mageuzi ya Rais Robert Mugabe, kama vile mageuzi ya katika sekta ya kilimo ambayo yaliathiri sekta muhimu ya uchumi wa nchi.

"Mikataba itawekewa saini, hasa katika kilimo, usafiri na miundombinu", amesema Joey Bimha, Katibu dola kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Zimbabwe, katika mahojiano na gazeti la kila siku la Herald, linalounga mkono serikali.

"Viongozi wengi wa makampuni ya China watakutana na wafanyabiashara wa Zimbabwe na hii itapelekea zaidi uwekezaji wa China kuinua zaidi biashara na faida zaidi kiuchumi kwa Zimbabwe", Joey Bimha ameongeza.

Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 91, ambaye anatuhumiwa mara kwa mara ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwakandamiza wapinzani wake, hata hivyo, alishinda tuzo ya Amani ya Confucius mwezi Oktoba, tuzo mbadala ya Nobel inayotolewa na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.