Pata taarifa kuu
VATICAN-AFRIKA-KENYA-MARIDHIANO

Papa alaani msimamo mkali wa vijana katika "mashambulizi ya kikatili"

Papa Francis amelaani na kukemea Alhamisi hii mjini Nairobi, hatua ya kwanza ya safari yake barani Afrika, msimamo mkali wa vijana katika "mashambulizi ya kikatili" na vurugu wakidai kuyatekeleza kwa jina la Mungu.

Papa Francis akitoa hotuba mjini Nairobi Novemba 25, 2015.
Papa Francis akitoa hotuba mjini Nairobi Novemba 25, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jina la Mungu halimaanishi chuki na vurugu", Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani amesema mbele ya viongozi wa dini nchini Kenya - Waislamu, Waprotestanti na Waanglikana.

Papa Francis Amekemea tabia ya "vijana kuwa na msimamo mkali wakidai kuwa wanafanya hivyo kwa imani za dini" ili kutenda "mashambulizi ya kikatili" akitoa mfano wa mauaji ya Westgate, Garissa na Mandera.

Papa Francis ataadhimisha Misa katika Chuo Kikuu cha Nairobi Alhamisi hii, ambapo siku hii imetangazwa kuwa likizo ya kitaifa. Askari polisi elfu kumi wamewekwa katika maeneo mbalimbali kwa usalama wa Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani.

Katika hotuba aliyoitoa mara baada tu ya kuwasili kwake kwenye Ikulu, makazi rasmi ya Rais Uhuru Kenyatta, Papa amewataka viongozi wa dunia kulinda mazingira na kutetea maendeleo endelevu kwa kufikiria vizazi vijavyo. Papa Francis amepanda mti katika bustani ya makazi ya rais.

Papa Francis pia atazungumzia suala la tabia nchi Alhamisi wiki hii katika hotuba yake kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.

Katika hotuba yake Ikulu, Papa Francis amewatolea wito "wanaume na wanawake wote wenye nia nzuri njema kujihusisha na masuala ya maridhiano, amani na msamaha" dhidi ya "mgawanyiko wa kikabila, kidini na kiuchumi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.