Pata taarifa kuu
NIGER-SHAMBULIZI-USALAMA

Niger: Boko Haram yaua wanakijiji 18 Gogone

Shambulio jingine la kigaidi limetokea Kusini-Mashariki mwa Niger, karibu na mpaka na Nigeria. Shambulio hilo linahusishwa wanajihadi wa kundi la Islamic State, kundi la kiislamu la Afrika Magharibi, linalojulikana kama Boko Haram.

Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015.
Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015. AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

Wanakijiji kumi na nane wameuawa, wengi wamejeruhiwa na zaidi ya nyumba mia moja zimechomwa moto.

Mashambulizi ya Gogone yalidumu karibu masaa mawili Jumatano Novemba 25. Yalitekelezwa na idadi kubwa ya wapiganaji wa Boko Haram. Nyumba sabini zilichomwa moto, Meya wa Bosso aliyetembelea kijiji hicho, amesema. Mamadou Bako amesema kuwa watoto wawili waliteketea kwa moto, watu kumi na mmoja wamejeruhiwa, wanne wako katika hali mbaya.

Wanakijiji walijihami kwa pinde na mishale dhidi ya wapiganaji wenye bunduki aina ya Kalashnikov, amesema mkuu wa mkoa, ambaye alitembelea eneo hilo. Hasara ni kubwa, Abdou Kaza amehuzunika.

Wapiganaji waliondoka katika kijiji cha Gogone kwa mguu, kijiji ambacho kinapatikana kilomita kumi na tano kutoka mji wa Bosso, lakini hasa mita kumi kutoka Mto Yobe, ambao unagawa mpaka wa asili kati ya Niger na Nigeria. Watu waliojeruhiwa walisafirishwa katika mji wa Diffa.

Bunge mwezi uliopita liliongeza muda wa hali ya hatari katika jimbo hilo la Kusini-Mashariki mwa Niger ambapo kundi la Boko Haram limezidisha mashambulizi yanayoendelea kusababisha vifo vya watu wengi. Mwezi uliopita wapiganaji hao waliwachinjwa wanakijiji kumi na mmoja katika kijiji kilio karibu na mji wa Diffa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.