Pata taarifa kuu
NIGERIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Nigeria: watu 15 wauawa katika shambulio Kano

Watu kumi na tano wameuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili yaliyotokea Jumatano wiki hii katika soko la mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria.

Polisi ya Nigeria katika eneo la shambulizi la kujitoa mhanga, Februari 24, 2015, Kano.
Polisi ya Nigeria katika eneo la shambulizi la kujitoa mhanga, Februari 24, 2015, Kano. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yametekelezwa nawasichana wawili waliojitoa mhanga kwa kujilipua, ambapo mmoja anakisiwa kuwa na umri wa miaka kumi , polisi imesema.

"Basi ndogo lililokua likisafirisha wanawake liliwasili katika soko maalumu la simu za mkononi (Farm Center GSM), kisha wasichana wawili, mmoja mwenye umri wa miaka 11 na na mwengine 18 walishuka kutoka katika basi, huku wote wawili wakiwa wamevaa hijab (hijabu)”, msemaji wa Polisi ya jimbo la Kano, Musa Magaji Majia, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Mmoja aliingia ndani ya soko, mwengine alibaki nje na kisha wakajilipua. watu waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini , lakini tumepata taarifa muda si mrefu kuwa watu kumi na tano ndio wamepoteza maisha, bila kuhesabu washambuliaji waliojitoa mhanga ", Musa Magaji Majia ameongeza

Mashambulizi hayo pia yamewajeruhiwa watu 53, ambapo wengi walitibiwa na waliweza kupewa ruhusa ya kuondoka hospitali, amesema msemaji wa polisi.

Mashambulizi haya ya kujitoa mhanga yanatokea siku moja baada ya shambulizi jingine lililowaua watu 30 katika mji wa Yola, kaskazini-mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.