Pata taarifa kuu
FIFA-UCHAGUZI-SOKA

Wagombea kwenye nafasi ya rais wa FIFA wajulikana

Shirikisho la Soka duniani (FIFA) limeidhinisha majina ya watu watano kati ya saba walioomba nafasi ya kuwania urais wa Shirikisho hilo wakati wa uchaguzi mpya utakapofanyika mwezi Februari mwaka ujao.

Mpiga picha akisubiri nje ya makao makuu ya FIFA, Oktoba 20, 2015, Zurich.
Mpiga picha akisubiri nje ya makao makuu ya FIFA, Oktoba 20, 2015, Zurich. AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Wagombea walioidhinishwa ni pamoja na Mwanamfalme wa Jordan Ali Al Hussein, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, Jerome Champagne, Gianni Infantino na Tokyo Sexwale raia wa Afrika Kusini.

Kamati ya nidhamu na maadili inasema hatima ya Mitchel Platini, rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya aliyesimamishwa kwa siku tisini kutojihusisha na maswala ya soka kwa tuhma za ufisadi, itafahamika baada ya muda huo kukamilika.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bility, ndio mgombea pekee ambaye hadi sasa ameondolewa kabisa katika kinyang’anyiro hicho.

Kamati hiyo ya FIFA inasema imemwondoa Bility katika orodha hiyo kwa sababu ya kuwa na rekodi mbaya ya nidhamu.

Platini ambaye amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo, huenda akapewa nafasi ya kugombea ikiwa atapatikana bila kosa kuhusu tuhma za kupokea Dola Milioni 2 kutoka kwa rais wa FIFA Sepp Blatter mwaka 2011.

Mawakili wa Platini wanasema wanasikitishwa mno na FIFA kwa namna inavyochukua muda mrefu kuamua hatima yake.

Mitchel Platini ameendelea kusisitiza kuwa hana kosa lolote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.