Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Afrika

IS yathibitisha kuhusika katika udunguaji wa ndege ya Urusi

media Un morceau de la carlingue de l'airbus de la compagnie russe, le 1er novembre 2015, après qu'il s'est écrasé dans le désert du Sinaï. KHALED DESOUKI/RUSSIA'S EMERGENCY MINISTRY/AFP

Kundi la Islamic State limethibitisha kwa mara nyingine tena Jumatano hii kuhusika katika udunguaji wa ndege ya Urusi nchini Misri katika jangwa la Sinai, lakini hakuna ushahidi mpya ambao umekuja kuthibitisha madai hayo.

Kundi hilo la kijihadi pia, hata hivyo, limekiri kuendesha shambulio jipya dhidi ya polisi wa Misri katika eneo la Sinai.

Wakati huo huo mjini Cairo, wataalam wameendelea kuchunguza vinasa sauti viwili vya ndege, ambapo kimoja kinahifadhi sauti na mazungumzo katika chumba cha marubani na kingine kinahifadhi vigezo vya ndege ikiwa angani. Wataalam hao wana matumaini kuwa vinasa sauti hivyo vitapelekea kuamua kati ya nadharia mbili ziliondekezwa ili kueleza ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 224: shambulio au ajali ya kiufundi.

Ujumbe mfupi wa sauti uliyorushwa kwenye akaunti ya yake ya Twitter ya kawaida, tawi la Islamic State, "Mkoa wa Sinai", limethibitisha kwa mara nyingine tenakuhusika katika udunguwaji wa ndege hiyo ya Urusi, siku tano baada ya kutangaza kuwa liliidungua ndege ya Urusi katika jangwa la Sinai.

Katika ujumbe mwingine kwenye Twitter, kundi hilo la kijihadi limekirii kuendesha shambulizi Jumatano hii asubuhi na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, ambae aamelipua gari lililokua limetegwa bomumbele ya klabu ya polisi katika mji wa Al-Arish, mji mkuu wa jimbo la Sinai Kaskazini, na kuwaua askari polisi 4, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

Kundi la "Mkoa wa Sinai", ambalo ;imekua likiendesha kila siku mashambulizi yanayowalenga askari polisi na wanajeshi, limebaini kwamba shambulizi hilo limeendeshwa katika kulipiza kisasi kwa "kukamatwa kwa wanawake wa Kibedui na vikosi vya usalama" katika mkoa huo.

Sisi ziarani London

Ni kwa hali hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameondoka Cairo Jumatano wiki hii kwa ziara ya siku tatu mjini London, kwa mujibu wa shirika la habari la Mena.
Katika mazungumzo ya simu, Rais Abdel Fatah al-Sisi amekubaliana na Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron juu ya haja ya "kuhakikisha usalama tosha" katika uwanja wa ndege wa Sharm el-Sheikh, ambapo ndege ya Urusi liyofanya ajali ilipaa ikielekea St Petersburg, viongozi wa Uingereza wamebaini.

Uwanja huo wa ndege unapokea kila siku maelfu ya watalii wanaokuja likizo katika mwambao wa Bahari ya Shamu.

Hayo yakijiri uchunguzi wa yaliyo katika vinasa sauti vya ndege ya Urusi ndege iliyoanguka nchini Misri, utaratibu muhimu kuamua kama ilifanya ajali ya kawaida au iilishambuliwa, unaweza kuchukua muda mrefu, maafisa wa timu ya uchunguzi wamebaini.

Hakuna ushahidi wa kutosha juu ya sababu ya ajali ya Airbus A321 ya Urusi uliojitokeza mpaka sasa, viongozi wanasubiri kupata ushahidi kamili kutoka vinasa sauti viwili vya ndege, au "masanduku meusi", ambapo moja inahifadhi mazungumzo na sauti nyingine zinazosikika katika chumba cha marubani na nyingine inahifadhi vigezo vya ndege ilio angani.

Uchunguzi wa vinasa sauti vya ndege ulianza Jumanne wiki katika makao makuu ya wizara ya Usafiri wa Anga ya Misri, afisa mwandamizi wa wizara hiyo ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwa masharti ya kutotajwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana