Pata taarifa kuu
URUSI-MISRI-AJALI YA NDEGE

Ajali ya ndege Sinai, hakuna aliyenusurika

Ndege ya abiria ya Urusi imeanguka katika Peninsula ya Sinai nchini Misri muda mfupi baada ya kupaa angani kutoka mji wa mapumziko wa Sharm el-Sheikh. Katika ndege hiyo waalikuwa watu 224, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi saba wa ndege hiyo.

Uwanja wa Ndege wa St Petersburg, Jumamosi, Oktoba 31, 2015. Familia za abiria waliokua wakisafiri katika ndege ya shirika la  Kogalymavia wakipewa taarifa kuwa hakuna abiria aliyenusurika.
Uwanja wa Ndege wa St Petersburg, Jumamosi, Oktoba 31, 2015. Familia za abiria waliokua wakisafiri katika ndege ya shirika la Kogalymavia wakipewa taarifa kuwa hakuna abiria aliyenusurika. REUTERS/Peter Kovalev
Matangazo ya kibiashara

Hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo. Kisanduku cheusi kimeoneka eneo kilipoangukia. Nchini Urusi, uchunguzi umeanzishwa dhidi ya kampuni ya Kogalymavia. Rubani alitaarifu mapema matatizo ya kiufundi kwa maafisa wa uwanja wa ndege kabla ya kupoteza mawasiliano.

Ndege hiyo ya Urusi iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa Sharm el-Sheikh, pembezoni mwa Bahari ya Shamu, 9:51 (saa za kimataifa). Ilikua inakwenda St Petersburg. katika ndege hiyo walikuwa wakisafiri watu 224: abiria 217 (ikiwa ni pamoja na raia ws tatu wa Ukraine), watoto kumi na saba na wafanyakazi saba. taarifa hii ya kuanguka kwa ndege ya Urusi imethibitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, Sherif Ismail, ambaye mara moja alikwenda wenye eneo la tukio, mwandishi wetu Cairo, Alexandre Buccianti, amearifu.

Mawasiliano ya rada ya ndege yenye chapa 7K 9268 pamoja na viongozi wa mamlaka ya ukaguzi wa anga yamepotea dakika 23 baada ya ndege hiyo kuondoka, amebaini Sergei Isvolski, msemaji wa mamlaka ya safari za ndege ya Urusi, akinukuliwa na Interfax.Ndege hiyo ilikua kwenye umbali wa mita 9500 kwenda juu. Ndege hiyo iliyo na namba ya usajili Kgl-9268 ni ndege ya abiria A321 ya shirika la ndege la Kogalymavia / Metrojet, ambayo makao yake makuu yako Magharibi mwa Siberia.

Jaribio la kutua kwa dharura

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka uwanja wa ndege wa Cairo, rubani alitaarifu kwa maafisa wa uwaja wa ndege matatizo ya kiufundi ya injini za ndege hiyo. Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, rubani alijaribu kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa al-Arish unaopatikana kilomita sitini kaskazini ya eneo la ajali.

Mabaki ya ndege yameonekana katika eneo la milima ya al-Hassana, katikati ya penensula ya Sinai. Ndege hiyo imeteketea kabisa, kwa mujibu wa vyombo vya usalama, ambavyo vimezingira eneo la ajali. Kwa mujibu wa gazeti la Misri Al-Ahram, hali ya hatari ilitangazwa na idara ya matibabu ya kaskazini mwa Sinai. Waziri mkuu wa Misri ameunda kwa ushirikiano na wizara na viongozi husikakitengo kitakachoendesha uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo.

Si mara kwanza kunashuhudiwa katika mji wa Misri wa Sharm el-Sheikh janga baya kama hili. Mika kumi na moja iliyopita , Januari 3, 2004, ndege ya shirika la Flash Airlines ilianguka baharini baada ya kupaa angani. Watu 148 walikuemo katika ndege hiyo walifariki, raia 134 wa Ufaransa walikua miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

IS yakiri kuiangusha ndege ya abiria ya Urusi

Kundi la Islamic State Group (IS) limedai kuwa wapiganaji wake ndio wameidungua ndege hiyo ya Urusi. Wanajihadi wanasema wamefanya hivyo katika kulipiza kisasi kwa Urusi ambayo imeingilia kijeshi nchini Syria kusaidia majeshi ya Bashr al Assad, lakini serilaki ya Moscow, kupitia Waziri wake wa Usafiri, Maxim Sokolov, imesema madai ya IS " hayawezi kuchukuliwa kuwa ya kweli. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.