Pata taarifa kuu
Nigeria Usalama

watu 7 wapoteza maisha jijini Maiduguri

Takriban watu 7 wamepoteza maisha katika mashambulio matatu yaliotekelezwa kwa wakati mmoja kwenye maeneo tofauti katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa nchi ya Nigeria.

AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Nigeria Kanali Sani Usman amesema mashambulizi yamefanyika na kupishana kwa dakika 3 na kuwauwa watu 7 wakiwemo waliotekeleza mashambulizi hayo. Watu wengine 11 wamejeruhiwa.

Licha ya kwamba hakuna kundi lolote lilijigamba kuhusika na mashambulizi hayo, kuna ishara tosha kwamba ni kundi la Boko Haram ndilo linalo husika na ambalo limezidisha mashambulizi dhidi ya raia.

Mashambulio hayo yamefanyika jana usiku katika kata ya Ajilari Cross, eneo lililolengwa mara mbili Septemba 20 mwaka huu katika mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu 117.

Octba mosi mwaka huu watu 10 walipoteza maisha na wengine 39 wakajeruhiwa baada ya washambuliaji kujilipua katika kata hiyo ilio karibu na uwanja wa ndege wa maiduguri na kambi ya kijeshi.

Mashambulizi ya kundi la Boko Haram yamesababisha vifo vya watu elf 17 na wengine zaidi ya milioni 2 kukimbia makwao tangu mwaka 2009 na wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya watu 1.300 tangu kuteuliwa kwa rais Muhamadou Buhari Mei 29 mwaka huu.

Jeshi la Nigeria limefaulu kukabiliana na wapiganaji wa kundi hilo, hadi kuwaokoa mateka kadhaa na kuonekana kulidhoofisha kundi hilo, lakini hivi karibuni Boko haram limezidisha mashambulizi ya kujitoa muhanga.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.