Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

Blater na Platini wasimamishwa kazi na kamati ya Nidhamu ya FIFA

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imechukua uamzi wa kuwasimamisha kazi rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter na rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya, Michel Platini.

Issa Hayatou,raia wa Cameroon, rais mpya wa mpito wa FIFA .
Issa Hayatou,raia wa Cameroon, rais mpya wa mpito wa FIFA . AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Nidhamu ya FIFA imemteuwa rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika Issa Hayatou kuwa kaimu rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Sepp Blatter na Michel Platini wanatuhumiwa kashfa ya ufisadi katika shirikisho hilo. Kabla ya uamzi wa FIFA, wawili hao walikua wakitupiana vijembe, kila mmoja akimtuhumu mwengine na kupinga kuendelea kushikilia wadhifa wowote katika taasisi za Soka ulimwenguni.

Sepp blatter amesimamishwa kazi kwa muda wa suku 90. Kaimu rais wa FIFA, Issa Hayatou , ambaye ni raia wa Cameroon, ameelezea furaha yake kuona anashikilia kwa muda Shirikisho hilo la Soka Duniani.

Hata hivyo wengi wanaona kuwa kuteuliwa kwa Issa Hayatou kwenye uongozi wa FIFA, kunampa nguvu aliyekuwa rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter, kwani Hayatou ni mshirika wa karibu wa Blatter.

Labda siku hata kabla ya 90. Sepp Blatter na wenzake waliosimamishwa kuna uwezekano wa kukata rufaa. Yeye na wengine waanaweza kutetea sababu zao.

Isasa Hayatou, mwenye umri wa miaka 69, kabla ya kuteuliwa kuwa kaimu rais, alikua mwenyekiti wa kamati ya fedha kwenye Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Hatua hii inakuja baada ya viongozi wa Mashtaka nchini Uswizi kumchunguza Blatter kwa tuhma za kutoa malipo yasiyokuwa rasmi kwa rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), Michel Platini, lakini kutoa saini mkataba ambao haukuwa na manufaa kwa FIFA.

Awali Blatter alikanusha tuhma hizo na kusema hana hatia yoyote na hawezi kujizulu kabla ya tarehe 26 mwezi Februari mwaka ujao siku ambayo uchaguzi mpya wa FIFA utakapofanyika.

Michel Platini naye, awali alisema fedha alizolipwa alikuwa amezifanyia kazi na hajahusika na ufisadi.

Hayo yakijiri kamati tendaji ya Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, imesema inamuunga mkono Michel Platini. haijafahamika iwapo kamati hiyo itakataa rufaa dhidi ya uamzi wa FIFA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.