Pata taarifa kuu
KENYA-EL-NINO-HALI YA HEWA-USALAMA

Watalamu waonya kutokea kwa mvua za El Nino Kenya

Watalaam wa utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya wameonya kuwa mvua za El Nino zinatazamiwa kuanza kunyesha Jumatano wiki hii katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Mjini Mombasa. Kamishena wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amewataka watu wanaoishi katika mitaa iliyo mabondeni kuhama
Mjini Mombasa. Kamishena wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amewataka watu wanaoishi katika mitaa iliyo mabondeni kuhama Sandro Senn/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Watu wanaoishi mabondeni na karibu na mito wameombwa kuhama.
Maeneo yatakayoathiriwa zaidi ni Pwani, Magharibi mwa nchi hiyo na eneo la Bonde la Ufa.

Kamishena wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amewataka watu wanaoishi katika mitaa iliyo mabondeni kuhama.

Mataifa yote ya Afrika Mashariki yanatarjiwa kushuhudia mvua hizo zinayokadiriwa kudumu kwa miezi miwili na wito kama huo umekuwa ukitolewa kwa wananchi wa nchi hizo kuwa makini.

Hayo ya kijiri, wanafunzi zaidi ya 500 wanaoshikiliwa katika makao makuu ya polisi mjini Eldoret nchini Kenya, wanatazamiwa kupandishwa kizimbani baadaye Jumanne hii.

Polisi iliwakamata wanafunzi hao mwishoni mwa juma kufuatia operesheni maalumu waliyoifanya usiku kwenye kumbi mbalimbali za starehe mjini Eldoret, ambapo walikamatwa wakiwa na miraa, bangi, vilevi huku mipira ya kiume (Condom) ikiwa imetapakaa kwenye ukumbi huo.

Polisi imesema waliwakamata wanafunzi hao baada ya kupokea taarifa kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakitumia kumbi hizo kuvutia bangi, miraa na kujihusisha na ngono.

Operesheni hii imefanyika ikiwa ni miezi 2 tu imepita toka wanafunzi wengine 40 wakamatwe katika basi mjini Nyeri, wakitumia dawa za kulevya na kujihusisha na ngono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.