Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Burkina Faso: viongozi wapongeza kurejeshwa kwa taasisi za mpito

media Rais Michel Kafando ni akisalimiwa na Boni Yayi katika sherehe ya kurejeshwa mamlakani, Septemba 23, 2015. AFP PHOTO / AHMED OUOBA

Wakati ambapo ujumbe wa marais kadhaa wa nchi za Afrika Magharibi uliwasili Jumatano wiki hii katika mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, rais wa mpito Michel Kafando amerejeshwa rasmi mamlakani baada ya kulihutubia taifa.

Wakati huo huo jenerali Gilbert Diendéré kiongozi wa wanajeshi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi amewaomba rasmi msamaha raia wa Burkina Faso.

Wadau wote wanaonekana kuridhika na kurudi kwa hali ya kawaida nchini Burkina Faso.

Rais mpito Michel Kafando ambaye alinga'tuliwa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi ya Septemba 17 amerejeshwa rasmi malakani Jumatano wiki hii. Wakati wa sherehe ya kurasimisha kurudi kwake madarakani, alipongezwa. Michel Kafandoamethibitisha nia yake kwa kutimiza kazi yake vizuri, ile ya kuiongoza Burkina Faso katika mchakato wa mpito baada ya utawala wa Blaise Compaoré.

" Naweza kuwahakikishia kwamba tutabaki na nia ya kuendelea na majukumu ambayo tulipewa na raia wa Burkina Faso. Majukumu ya kuweka taasisi za kuaminika na ya haki kwa ajili ya kuijenga upya Burkina Faso, na tumejikubalisha kwa nia njema kuijenga katika msingi wa demokrasia, na kuboresha vyomba vya sheria. Msimamo wa vijana wetu, msimamo wa jumuiya ya kimataifa na mataifa jirani kwa kulaani mapinduzi ya kijeshi, misimamo yote hiyo imetupa faraja na kuwa na matumani kwamba kazi tunayoifanya inapongezwa na ulimwengu mzima. Kwa hiyo hata iweje, na licha ya uvumilivu na ghadhabu ya vikosi vya uovu, tutaendelea kukabiliana na changamoto ", amesema Rais wa mpito Michel Kafando katika hotuba yake

Hata hivyo Bénéwendé Sankara, kiongozi wa chama cha upinzani cha UNIR / PS ametioa hisia zake baada ya hotuba ya Rais Kafando: " Mimi najivunia kuwa mwananchi wa Burkina Faso, najivuniakuwa mwanachamawa jumuiya ya ECOWAS, najivunia kuwa Mwafrika, najivunia kuwa mwanaharakati wa uhuru, wa haki, na mtetezi wa demokrasia. Nadhani ni katika umoja zaidi ambao umepelekea tupate ushindi kwa pamoja. Tumeweza kupata ushindi huu kwa sababu pia jumuiya ya kimataifa ina nia ya ukweli, haki na maadili ya demokrasia. "

 Burkina Faso yarejea katika hali yake ya kawaida

Katika mji mkuu wa Burkina Faso, hali ya kawaida imerejea licha ya kuwepo kwa kiasi kikubwa cha wanajeshi Lakini wengi sasa wanadai uwajibikaji, na maeneo mengine ya nchi, mitaani bado ni hasira, hata baada kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi kuomba msamaha wananchi wa Burkina Faso kwa yale yaliyotokea.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana