Pata taarifa kuu
MEXICO-MISRI-SHAMBULIZI-USALAMA

Misri: Mexico yalaani shambulizi la jeshi dhidi ya raia wake

Jumatatu wiki hii Mexico imeeleza " kuskitishwa " na kutoa wito kwa " uchunguzi wa haraka, na wa kina " baada ya shambulizi la anga la jeshi la Misri lilowauawatalii wawili kutoka Mexico.

Claudia Ruiz Massieu, waziri wa mambo ya nje wa Mexico, akilaani shambulizi la jeshila Misri dhidi ya watalii kutoka Mexico.
Claudia Ruiz Massieu, waziri wa mambo ya nje wa Mexico, akilaani shambulizi la jeshila Misri dhidi ya watalii kutoka Mexico. Photo par MOHAMED EL-SHAHED/AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Misri hawakueleza bayana ni silaha gani iliyotumiwa katika shambulizi la Jumapili katika eneo la madharibi mwa Jangwa la Misri, ambapo watu 12, ikiwa ni pamoja na raia wa Mexico wawili waliuawa na 10 kujeruhiwa.

Lakini kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Mexico, Claudia Ruiz Massieu, manusura sita kutoka Mexico walimwambia Balozi wa Mexico nchini Misri kwamba walilengwa na " shambulizi la angani la mabomu yaliyorushwa kutoka ndege na helikopta " wakati ambapo walikua wakipumzika ili wapate chakula cha mchana.

" Serikali ya Mexico imewataka viongozi wa Misri kuanzisha uchunguzi haraka iwezekanavyo na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na shambulizi hilo ", amesema Ruiz Massieu.

Watalii sita wa Mexico waliojeruhiwa na kupelekwa hospitalini mjini Cairo,wanaendelea vizuri, kwa mujibu wa Waziri Claudia Ruiz Massieu .

Kundi la watalii waliwasili mjini Cairo tarehe 11 Septemba na waliondoka siku mbili baadaye kuelekea Bahariya Oasis, amesema Ruiz Massieu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.