Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Zaidi ya watu 15 wauawa katika shambulio kaskazini mwa Cameroon

media Mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 15 katika mji wa Kerawa, Kaskazini mwa Cameroon. Reinnier KAZE / AFP

Alhamisi wiki hii kumetokea shambulio karibu na kambi ya jeshi, katika mji wa Karewa, kaskazini mwa Cameroon, shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu kumi na tisa na wengine 143 wamejeruhiwa.

Vikosi vya serikali vinaendelea na mapigano dhidi ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kutoka Nigeria.

Wakati huo huo shambulio jingine limetokea katika soko la mji, vyanzo vya kijeshi vimeeleza

" Kwa sasa, kunaripotiwa zaidi ya watu kumi natano wameuawa na zaidi ya mia moja wamejeruhiwa katika shambulio lililotokea karibu na kambi (...) Tunasubiri ripoti ya timu yetu kuhusu shambulio la pili lililotokea katika soko ", amesema afisa anayehudumu katika eneo hilo.

Askari polisi wa mji huo amethibitisha idadi hiyo, lakini mfanyakazi mmoja wa serikali amethibitisha kuwa shambulio hilo limewaua watu sita na wengine 87 wamejeruhiwa.

Bomu la kwanza limelipuka sokoni, kisha la pili limechomwa moto karibu na kambi ya jeshi ambapo wanapigakambi wanajeshi wa kikosi kilichotengwa kwa kupambana dhidi ya Boko Haram.

Upande wa mpaka wa Nigeria, shambulio katika kijiji cha Borno, kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo, liliwaua watu watano na kuwajeruhi wengine sita Jumatano wiki hii, vyanzo vya kijeshi vimebaini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana