Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Burundi: Nkurunziza apania kufanya marekebisho ya Katiba

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesisitiza Alhamisi wiki hii kuwa waasi wa nchi yake wataangamizwa na Mungu baada ya yeye kuapishwa katika muktadha wa utata wa awamu yake ya tatu.

Wakati wa kuapishwa kwake, Agosti 20 mwaka 2015, Pierre Nkurunziza alielezea nia yake ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.e.
Wakati wa kuapishwa kwake, Agosti 20 mwaka 2015, Pierre Nkurunziza alielezea nia yake ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.e. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Nkurunziza ameyasema hayo wakati wa hotuba yake ya uzinduzi pamoja na kuahidi kufanya marekebisho ya kikatiba kwa baadhi ya Ibara ikiwa ni pamoja na Ibara ya 129 ya Katiba na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Msemaji wa rais Pierre Nkurunziza, Grvais Abayeho amebainisha umuhimu wa mabadiliko ya sheria zinazosimamia taasisi zisizo za kiserikali na mashirika ya kiraia yanayojichanganya na siasa kinyume na inavyotarajiwa. Abayeho amesema ni lazima sheria ifwate mkondo wake.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaendelea kuamini kuwa licha ya rais Nkurunzia kuapishwa, bado hajawa na uhalali wa kisiasa kuongoza nchi hiyo.

Sherehe hizo za kuapishwa kwa Nkurunziza zinaendelea kuzusha maswali kwa vile hapakuwepo na kiongozi yeyote wa kikanda na sherehe hizo kutangazwa ghafla kinyume na ilivyotarajiwa.

Wakati huo huo Leonard Nyangoma, kiongozi mkuu wa upinzani aliyechaguliwa hivi karibuni nchini Ethiopia, kuongoza muungano na mashirika ya kiraia yanayopinga muhula wa tatu wa Nkurunziza, ambao majukumu yake, kulingana na muungano huo yatakua sambamba na utawala wa Nkurunziza, amemuonya rais huyo kujiuzulu kabla ya tarehe 26 Agosti mwaka 2015, la si hivyo atakiona cha mtima kuni.

Hayo yakijiri hali ya wasi wasi imeendelea kutanda nchini humo, hasa katika mji mkuu Bujumbura. raia wana hofu ya kutokea kwa vita, baada ya idadi kubwa ya wanajeshi wa zamani kutoka kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani kulitoroka jeshi la nchi hiyo, na kuingia maguguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.