Pata taarifa kuu
BOKO HARAM-NIGERIA-CHAD-USALAMA

Boko Haram: Shekau awajibu marais wa Nigeria na Chad

Katika ujumbe wa sauti, Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Islamic State Afrika Magharibi (Boko Haram) amekanusha taarifa zozote zinazolenga kumdhohofisha zikisema kuwa aliuawa majuma kadhaa yaliopita. Shekau amemuonya rais wa Chad Idriss Deby ambaye alisema kuwa kundi lake lilisambaratishwa.

Kiongozi wa kundi la zamani la Boko Haram, Abubakar Shekau.
Kiongozi wa kundi la zamani la Boko Haram, Abubakar Shekau. AFP/Capture d'écran vidéo
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo Shekau ameutoa katika lugha ya Kihausa. Sauti hiyo yenye dakika nane imetambuliwa na wataalam wa kundi la zamani la Boko Haram lilobadili jina na kuitwa Islamic State Afrika Magharibi kama ile ya Abubakar Shekau. Shekau, haiko tena hai na kundi lake limesambaratika, wamedai marais Idriss Déby na Muhammadu Buhari.

" Unaweza kusoma na kusikia katika vyombo vya habari vya makafiri duniani kwamba mimi nimekufa au kwamba mimi ni mgonjwa na nimepoteza ushawishi wangu, lakini wanapaswa kufahamu kwamba si kweli. Ni uongo ", amesema Shekau. Kwa mujibu wa wataalamu katika masuala ya ujasusi, sauti hiyo imerekodiwa hivi karibuni, kwani inazungumzia matangazo ya hivi karibuni ya rais Deby na Buhari waliotoa tarehe 11 na 13 Agosti.

Akizungumzia rais wa Chad, Shekau amemtaja kuwa ni mnafiki na mjeuri. Akizungumzia rais wa Nigeria, kiongozi huyo wa Islamic State Afrika Magharibi amemuita "mtu anaye jifaharisha na mwongo". Muhammadu Buhari aliahidi Alhamisi kwa atahakikisha amelitokomeza kundi hilo la kiislamu katika kipindi cha miezi mitatu. Shekau amepuuzia na kusema kuwa " ni miaka mitatu sasa hamjafaulu kutuangamiza".

Katika ujumbe, uliyotolewa Jumapili Agosti 16, kiongozi huyo wa kijihadi ameongea mwenyewe kwa mara ya kwanza kuwa ni kiongozi wa tawi la Afrika Magharibi la Islamic State na kutoa heshima zake kwa Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la Islamic State. Islamic State, ambayo, kwa mujibu wa wataalam, sasa inasimamia kwa sasa mawasiliano ya kundi la zamani la Boko Haram. Ujumbe wa Shekau umetafsiriwa haraka katika lugha ya Kiarabu kwa ajili ya usambazaji mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.