Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAUAJi-USALAMA-SIASA

Burundi: mkuu wa zamani wa majeshi auawa

Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Burundi, kanali Jean Bikomagu, ameuawa Jumamosi Agosti 15 katika kata ya Kabondo, wilayani Kinindo, jijini Bujumbura.

Mji wa Bujumbura.
Mji wa Bujumbura. AFP/Carl de Souza
Matangazo ya kibiashara

Kanali Jean Bikomagu ni kutoka jamii ya Watutsi, ambaye alikua kiongozi wa majeshi wakati wa vita vya vita vya wenyewe kwa wenyewe (kati ya mwaka (1996-2006) dhidi ya waasi wa CNDD-FDD, ambao kwa sasa wako madarakani.

Kwa mujibu wa shahidi aliyenukuliwa na waandishi wa habari wa Burundi wanaochapisha habari zao kwenye mtandao wa intaneti, " kanali mstaafu alikuwa akirudi nyumbani kwake akiambatana na binti yake. Alipo wasili katika lango ili aweze kuingia nyumbani kwake akiwa ndani ya gari, watu waliokua kwenye pikipiki walimfyatulia risase yeye na binti yake, na baadae walitimka ". Jean Bikomagu alifariki papo hapo, binti yake amejeruhiwa na wakati huu amelazwa katika hospitali jirani ya Bumerec wilayani Rohero.

Kanali Jean Bikomagu ni miongoni mwa maafisa wa jeshi la zamani la Burundi lilokua na idadi kubwa ya wanajeshi kutoka jamii ya watu wachache ya Watutsi waliopigana dhidi ya makundi ya zamani ya waasi kutoka jamii ya watu walio wengi ya Wahutu, hasa waasi wa zamani kutoka CNDD-FDD. Siku chache baada ya waasi wa CNDD-FDD kushirikishwa katika taasisi za uongozi wa jeshi, ikiwa ni pamoja na jeshi na polisi, luteni jenerali Adolphe Nshimirimana, aliye kua karibu ya rais Pierre Nkurunziza, aliteuliwa kuwa mkuu wa majeshi. Luteni Adolphe Nshimirimana aliuawa, pia mchana, wiki mbili zilizopita, jijini Bujumbura. Uvumi umekua ukisambaa mjini Bujumbura kuwa luteni jenerali Adolphe Nshimirimana hatazikwa kabla hajauawa afisaa mwengine mwenye cheo kama chake kutoka jamii nyingine.

Kanali Jean Bikomagu alikua kwanza mkuu wa jeshi katika utawala wa rais Pierre Buyoya. Mwaka 1993, rais wa kwanza aliyechaguliwa nchini ya misingi ya kidemokrasia, kutoka jamii ya Wahutu, Melchior Ndadaye, alimbakiza kwenye wadhifa wake. Miezi michache baadaye, rais Ndadaye aliuawa katika jaribio la mapinduzi ya kijeshi. Baadhi walimshuku kanali Bikomagu kwa kuhusika katika mauaji hayo, lakini wakati huo kanali Jean Bikomagu alikanusha tuhuma hizo dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.