Pata taarifa kuu
UN-BURUNDI-SIASA-USALAMA

UN yaomba uchunguzi kuhusu shambulio dhidi ya Mbonimpa

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametaka uchunguzi wa kina ufanywe kwa shambulio lililofanywa dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi, Pierre-Claver Mbonimpa, kiongozi wa shirika la kutetea haki za binadamu na za wafungwa, APRODH.

Kiongozi wa shirika linalotetea haki za binadamu, APRODH, Pierre-Claver Mbonimpa.
Kiongozi wa shirika linalotetea haki za binadamu, APRODH, Pierre-Claver Mbonimpa. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Pierre-Claver Mbonimpa aliponea kuuawa baada ya kujeruhiwa kwa risasi alizovyatuliwa na mtu aliyekuwa kwenye pikipiki katika kata ya Kanga wilayani Kinama, Kaskazini mwa jiji la Bujumbura, jioni ya siku ya Jumatatu Agosti 3.

Hali ya wasiwasi imetanda katika mji wa Bujumbura na wakaazi wa mji huo wameingiliwa na hofu baada ya kusikia tukio hilo.

Uvumi wa kuuawa kwa Pierre-Claver Mbonimpa ulianza kuzagaa tangu Jumapili Agost 2 nchini Burundi. Lakini Jumatatu mchana wiki hii, mwanaharakati huyo amekanusha taarifa hiyo.

Saa zisiozidi nne baadae, yaani saa 12 na robo, mtu aliye kuwa kwenye pikipiki amemfyatulia risasi Pierre-Claver Mbonimpa wakati alipokua akirudi nyubani katika kata ya Carama wilayani Kinama, Kaskazini mwa jiji la Bujumbura.

Kwa mujibu wa mwanawe Mbonimpa, Amandine Nasagarare, hali ya afya ya baba yake imeimarishwa.

Wakati huo huo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda mjini Bujumbura, wakati ambapo kundi la watu wenye silaha waliokua katika gari ndogo aina ya Probox walishambulia Jumanne mchana wiki hii gari la kijeshi na kuwajeruhi wanajesi kadhaa karibu na kituo cha redio na televisheni vya taifa RTNB.

Hayo yakijiri milio ya risasi na milipuko ya magruneti imeendelea kusikia katika vilaya ya Cibitoke, Nyakabiga na Ngagara, jini Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.