Pata taarifa kuu
NIGERIA-CAMEROON-BOKO HARAM-USALAMA

Muhammadu Buhari na Paul Biya wazungumzia suala la Boko Haram

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anahitimisha Alhamisi wiki hii ziara ya kikazi iliokua ikisubiriwa nchini Cameroon. Alipowasili Jumatano wiki hii, alikutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Cameroon Paul Biya.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (kushoto) akipokelewa na mwenzake wa Cameroon Paul Biya mjini Yaounde, Julai 29 mwaka 2015.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (kushoto) akipokelewa na mwenzake wa Cameroon Paul Biya mjini Yaounde, Julai 29 mwaka 2015. AFP PHOTO / CAMEROON PRESIDENCY
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili walizungumza kwa muda mrefu kuhusu kuimarishwa kwa mikakati yao katika kupambana dhidi ya kundi la Islamic Tsate katika Afrika ya Magharibi (Boko Haram).

Nchi za Cameroon na Nigeria zilikua mara nyingi na misimamo tofauti. Ziara hii, ilivyoelezwa kama ya mashauriano ya kijeshi, itapelekea kutuliza mvutano na mzozo wa kimipaka uliokua ukishuhudiwa kati ya nchi hizi mbili.

Mazungumzo kati ya Muhammadu Buhari na Paul Biya yaligubikwa hasa na vita dhidi ya kundi la Islamic State katika Afrika Magharibi (Boko Haram). Viongozi wa nchi hizi mbili katika hotuba zao walisisitiza umuhimu wa kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kumshinda adui wao wa pamoja, ambaye ni kundi la kijihadi na kundi hili ni tishio kwa maendeleo endelevu ya nchi hizi mbili, wamesema marais hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.