Pata taarifa kuu
NIGERIA-CAMEROON-DIPLOMASIA-USALAMA

Rais wa Nigeria aanza ziara ya kikazi Cameroon

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatazamiwa kufanya ziara ya kikazi leo Jumatano nchini Cameroon. Nchi hizi mbili zina mahusiano haba kutokana na migogoro ya mipaka ya kihistoria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakukutana na mwenzake wa Cameroon Paul Biya Jumatano Julai 29 mwaka 2015.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakukutana na mwenzake wa Cameroon Paul Biya Jumatano Julai 29 mwaka 2015. AFP via telegraph
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, haja ya ushirikiano katika vita dhidi ya kundi la Islamic StateKiislamu katika Afrika Magharibi (Boko Haram) inaweza kuziunganisha nchi hizi mbili ambazo zina maslahi ya pamoja.

Ziara hii " ina lengo la kujenga ushirikiano wa kikanda wenye nguvu katika kukabiliana na kundi la kiislam ", kwa mujibu wa msemaji waIkulu ya rais wa Nigeria. Hata hivyo, Rais Paul Biya, madarakani tangu mwaka 1983, mwaka ambao Muhammadu Buhari aliipindua serikali iliokuwepo wakati huo, na tayari sasa wawili hao wanafahamiana. Swali ni kujua uhusiano kati ya Paul Biya na Muhammadu Buhari utakuwa mgumu kuliko ilivyokuwa pamoja na Goodluck Jonathan miaka mitatu iliyopita.

Mwaka 1984, Paul Biya aliepuka jaribio la mapinduzi. Harakati na mipango mbalimbali vinavyoendeshwa na baadhi ya watu kaskazini mwa Cameroon vinamchukiza Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari. Uhusiano kati ya viongozi hawa wawili sio mzuri sasa. Tangu miaka thelathini iliopita. Lakini uhusiano karti ya Cameroon na Nigeria bado ni tete. Mzozo wa kihistoria, unatokana na migogoro kadhaa ya mipaka.

Pia katika uhusiano huu tata, ishara ya mfano ni muhimu. Mjini Yaounde, walikua na tabia tangu miaka kumi na tano iliopita kuwa rais anayechaguliwa nchini Nigeria anapaswa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Cameroon, kabla ya nchi zingine za kigeni. Muhammadu Buhari atatumia fursa hiyo na kufanya ziara ya kikazi nchini Cameroon licha ya kukosolewa na baadhi ya watu mjini Yaoundé.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.