Pata taarifa kuu

Kwa ziara ya Obama, rais wa Kenya ataka kuboresha ushirikiano wake

Rais wa Marekani Barack Obama anatazamiwa kuwasili mjini Nairobi siku ya Ijumaa Julai 24, na Rais wa Kenya Jumanne wiki hii alielezea matarajio yake kwa ajili ya ziara ya Barack Obama nchini mwake.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Nairobi, Julai 21 mwaka 2015.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Nairobi, Julai 21 mwaka 2015. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Biashara na mapambano dhidi ya ugaidi ni mada mbili ambazo zitapewa kipaumbele, amesema Uhuru Kenyatta. Rais huyo amepuuzia athari za uhalifu wa kivita uliyokua ukimkabili. Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imeahirisha kesi yake kwa muda usiojulikana kwa kukosa ushahidi. Kwa sasa ziara ya Obama inakuja kusaiadia kurejesha sifa za rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2013, mwanadiplomasia mmoja wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika wa wakati huo alijaribu kukatisha tamaa wapiga kura wa Kenya kutowapigia kura Uhuru Kenyatta William Ruto. Wawili hao leo ni viongozi vigogo nchini Kenya. Rais wa Kenya na Makamu wa wake walikua walifunguliwa mashitaka na ICC kwa kuhusika kwao katika ghasia ziliyofuata uchaguzi wa mwaka 2007.

Lakini ukurasa huo umebadilika, amesema Uhuru Kenyatta Jumanne wiki hii. "Hakuna kitu kinachozikutanisha nchi zetu hizi mbili ispokua maadili ambayo tunachangia. Na wale wote ambao wameonyesha mashaka juu ya uewezekano wa ushirikiano na urafiki kati ya nchi zetu mbili wangelirejelea uchambuzi wao", ameonya rais wa Kenya.

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC ilifuta mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta mwezi Desemba mwaka 2014 kwa kukosa ushahidi, lakini makamu wake William Ruto, hajafutiwa mashtaka. Hii haitazuia kupeana mikono kati ya Obama na William Ruto, amesema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Mada hii imekua gumzo nchini Kenya. " Hakuna shaka kwamba Obama anakuja kukutana na serikali iliopo madarakani, ni kusema wajumbe wote wa serikali, kwa sasa hili suala halina nafasi wakati huu, kwani makamu wa rais ni mmoja wa wajumbe wa serikali hii, hivyo tutaweza kukutana sote na kinachohitajika wakati huu ni ushirikiano kati ya Kenya na Marekani ", amesema Uhuru Kenyatta.

Ulinzi nchini Kenya umeimarishwa ikisalia siku moja tu kalba ya kuwasili kwa rais wa Marekani Barack Obama. Mpaka sasa haijajulikana iwapo Obama atatembelea kijiji cha Kogelo alikozailwa baba yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.