Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-UCHAGUZI-USALAMA

Burundi: Uchaguzi wa urais kufanyika leo

Nchini Burundi, wapiga kura milioni 3.8 wametakiwa Jumanne wiki hii kuitikia uchaguzi wa urais wakati ambapo rais Pierre Nkurunziza atawania muhula wa tatu ambao umeendelea kuleta utata nchini humo.

Wafuasi wa rais Nkurunziza wakibebelea mabango yaliyowekwa picha yake katika wilaya ya Kabezi, Julai 3 mwaka 2015.
Wafuasi wa rais Nkurunziza wakibebelea mabango yaliyowekwa picha yake katika wilaya ya Kabezi, Julai 3 mwaka 2015. RFI/Richard Riffonneau
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unafanyika katika hali ya wasiwasi ya kisiasa baada ya kusitishwa kwa mazungumzo kati ya serikali na upinzani. Kama ilivyokua katika uchaguzi wa wabunge na madiwani Juni 29, upinzani umeamua kususia uchaguzi huu.

Marais wa zamani, Sylvestre Ntibantunganya na Domitien Ndayizeye, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa chama cha Frodebu Nyakuri, Jean Minani, walionesha msimamo wao, kwamba matokeo ya uchaguzi huo yatakua batili. Lakini kwa upande wake mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (Ceni), amesema zoezi la kuondoa faili zao kwenye Tume huru ya Uchaguzi halikufuata utaratibu. Wangelipaswa kila mmoja kuandika barua yake binafsi ya kuondoa faili zao kwenye tume huru ya Uchaguzi, amesema Pierre Claver-Ndayicariye.

" Hatutashiriki katika uchaguzihuu wa kuigiza na tunatoa wito kwa wafuasi wetu kususia uchaguzi huu ", wamesema viongozi hawa wa kihistoria katika siasa nchini Burundi.

Hata hivyo mshauri mkuu wa rais katika masuala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe amesema uamzi wa viongozi hao hauna uzito wowote wakati huu.

" Wakati wanajua kuwa hawana usemi wala nguvu yoyote wakati huu nchini, ni lazima watafute kisingizio cha kujiondoa katika uchaguzi", amesema Willy Nyamitwe.

Mpaka sasa inafahamika kuwa wagombea ni wanane katika uchaguzi wa urais, licha ya kujiondoa kwa baadhi ya wagombea kwa kususia uchaguzi huo. Ushindi wa rais Pierre Nkurunziza hauna shaka. Baada ya ushindi mkubwa wa chama chake, CNDD-FDD, katika uchaguzi wa wabunge na madiwani tarehe 29 Juni, Rais anayemaliza muda wake atashindana na wagombea watatu kutoka vyama vidogo ambayo ni washirika wa wa utawala wake. Mpaka sasa mpinzani wake kuu, Agathon Rwasa, hajaondoa faili yake ya kugombea uchaguzi wa urais kwenye Tume huru ya Uchaguzi, lakini kama wapinzani wengine ameendelea kupinga mazingira ambamo uchaguzi huo utafanyika, na uhalali wa uchaguzi huo, huku akiendelea kuomba uchaguzi uahirishwe.

Mashambulizi ya guruneti na milio ya risasi

Hayo yakijiri Jumatatu alaasiri wiki hii utawala wa Bujumbura ulikutana na mabalozi wa Umoja wa Ulaya, ambapo kulijitokeza mvutano kati ya pande hizi. Mabalozi wa Umoja wa Ulaya wameitaka serikali kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kutafutia ufumbuzi mgogoro unaendelea kushuhudiwa nchini humo. Mabalozi hao wameendelea kusema kuwa kuna hatari nchi ya Burundi kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wakati huo huo milio ya risasi na milipuko ya mabomu imeendelea kusikika Jumatatu jioni hadi usiku kucha mjini Bujumbura, hasa katika wilaya za Bwiza na Nyakabiga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.