Pata taarifa kuu
BURUNDI-EAC-USALAMA-SIASA

Burundi: serikali yajiondoa kwenye meza ya mazungumzo

Nchini Burundi mazungumzo yanayozijumuisha pande zote husika katika kutafutia ufumbuzi mgogoro unaoendelea nchini humo chini ya mwamvuli wa upatanishi wa Uganda yalikua yanatazamiwa kufunguliwa kwa siku ya nne Jumpili Julai 19.

Mazungumzo kuhusu Burundi: Waziri wa ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera.
Mazungumzo kuhusu Burundi: Waziri wa ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Lakini wawakilishi kutoka kambi ya rais hawakuwepo leo Jumapili asubuhi katika mazungumzo hayo, wala serikali wala chama tawala au washirika wake. Suala la kalenda ya uchaguzi ndilo lingeligubika mazungumzo ya siku ya leo Jumapili Julai 19, ikiwa zimesalia tu siku mbili kabla ya uchaguzi wa rais, ambao umepangwa kufanyika Jumanee Jula 21.

Jumamosi jioni mwishoni mwa juma hili, waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana alitangaza kwamba serikali haitoshiriki mazungumzo, mpaka ikutane. Alipoulizwa kuhusu kuanza kwa mazungumzo leo asubuhi, baada ya timu ya usuluhishi kutangaza kuanza kwa mazungumzo hayo, Edouard Nduwimana ameeleza kuwa ujumbe wake una majukumu mengine, kama vile uteuzi wa wakuu wa wilaya, misa na majukumu ya kijamii.

Jumamosi Julai 18 serikali ya Burundi iliomba kikao cha mazungumzo kisitishwe ili iweze kushauriana. Mawaziri wawili waliokuwepo katika mazungumzo hayo walisema kuwa waligundua kuwepo kwa hati iliotolewa siku kadhaa ziliopita, ambayo inaishushia lawama kambi ya rais na kuituhumu makosa mbalimbali ambayo yanaendana na mazungumzo hayo. Hati hiyo ilitiliwa saini na vyama kadhaa vya upinzani, ambayo inatoa wito wa maandalizi ya mkutano wa vyama vyote vya upinzani vya ndani na nje ya nchi, katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa...

Kambi ya rais ilizungumzia pia tangazo la kuundwa katika siku za usoni baraza la kitaifa kwa ajili ya kuulinda Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha, Mkataba ambao ulimalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Neno ambalo serikali inakosoa lililoandikwa katika tangazo hilo, linasema: " Baraza hilo litawajibika na jukumu lake halali la kusimamia sheria ya nchi na taasisi zote za uongozi wa nchi ".

Huu ni uthibitisho kiwa upinzani unaendelea na mpango wao wa mapinduzi ya serikali, wamesema wajumbe kadhaa wa kambi ya rais. Upinzani kwa upande wao umesema, ni wazi serikali haikuwa na nia ya kushiriki mazungumzo na inaendelea na ubabe wake nwa kulazimisha uchaguzi.

Timu ya usuluhishi imesema kuwa itaendelea na jitihada za kukutanisha pande zote husika ili kutafutia ufumbuzi mgogoro unaoendelea kushuhudiwa Burundi. Waziri wa ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga amesema masuala yote yaliyowekwa mezani ikiwa ni pamoja na muhula wa tatu wa rais Nkurunziza, usalama, wakimbizi, kalenda ya uchaguzi, ... vitajadiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.