Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-CHINA-SHERIA-DIPLOMASIA

Raia wa Afrika Kusini wakamatwa China

Wakati ambapo makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameanza ziara ya kikazi katika Beijing, raia wa Afrika Kusini wamekamatwa kaskazini mwa China wakati wa ziara ya kitalii. Watano miongoni mwao wanaweza hata kushitakiwa. China inawatuhumu kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi.

Raia wa Afrika Kusini wakamatwa wakati makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa katika zira ya kikazi China.
Raia wa Afrika Kusini wakamatwa wakati makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa katika zira ya kikazi China. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Afrika Kusini ina hofu na usalama wa raia wake. Kumi miongoni mwa raia wake walikamatwa hata kama Makamu wa rais wa nchi hiyo ameanza ziara ya kikazi nchini China. Maelezo yanatatanisha na serikali ya Afrika Kusini bado haielewi kinachoendelea.

Watu hao kumi wanaonekana kuwa walikua katika katika kundi la watalii walikua wakitembelea eneo la kaskazini mwa nchi, jimbo la Mongolia, wakati walikamatwa. Watu wengine miongoni mwa wanaounda kundi hili ni kutoka Uingereza na raia mmoja kutoka India.

" Ilikuwa safari ya kuchunguza China ya kale ", limeandika shirika la kiutu, Gift of the Givers, kwenye ukurasa wake wa Facebook Wafanyakazi ishirini wa shirika hili pia wamezuiliwa nchini China. Shirika hili lenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini limesema katika mtandao wake wa Intaneti kuwa " safari yao ilikua mbaya zaidi Ijumaa Julai 10 ".

Licha ya kuwa safari yao ilikabiliwa na matatizo mengi, watalii hao ikiwa ni pamoja na raia kumi kutoka Afrika Kusini, tisa kutoka Uingereza na mmoja kutoka India, waliwasili kwa shida katika uwanja wa Ordos katika jimbo la Mongolia, kabla ya kukamatwa.

Uhusiano na makundi ya kigaidi?

Masaa 48 tu baada ya shirika la safari za ndege kugundua kuwa kuna hali ya sintofahamu, amearifu mwandishi wa RFI Beijing, Heike Schmidt. "Watalii hao walipokonywa simu zao, na hawakuweza kuwasiliana na balozi zao au wala familia zao," shirika hilo limesema katika tangazo lake. Polisi inawatuhumu baadhi yao ku walikua wakiangalia " video ya propaganda " katika chumba kimoja cha hoteli waliyokuwemo na " kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.